MAHAKAMA YA KADHI HAITAHUDUMIWA NA SERIKALI AMESEMA MWANASHERIA MKUU
Mh. George Masaju amesema mahakama ya kadhi itakayoanzishwa kisheria haitahudumiwa na serikali.
Mwanasheria mkuu wa serikali Mh. George Masaju amesema mahakama ya kadhi itakayoanzishwa kisheria haitahudumiwa na serikali na itakuwa ya hiari kwa waumini wa dini ya kiislamu watakaoiridhia katika masuala ya ndoa, talaka, mirathi pamoja na wakfu na kutaka wanasiasa kuacha kukuza mijadala ya suala hilo kwa maslahi yao binafsi.

Akizungumza katika mahojiano maalum na vyombo vya habari vya IPP
Bw.Masaju amesema uwepo wa mahakama hiyo utaisaidia serikali katika
kuipunguzia mzigo wa mlundikano wa kesi uliopo hivi sasa hivyo ni bora
dini zote zikaiunga mkono.
Aidha mwanasheria mkuu huyo wa serikali amekiri madhaifu
yaliyofanywa na serikali ya kutotoa elimu kuhusiana na faida ya mahakama
ya kadhi kuwa yamechangia pia mjadala kuhusiana na uanzishwaji wake.
Kuhusiana uwepo wa mjadala huo kulenga kuifanya jamii iache
kujadili mambo yanayolikabili taifa ambayo ni upigaji kura ya maoni ya
katiba pendekezwa, uandikishwaji wa wapiga kura pamoja na uchaguzi mkuu
amesema.