Bukobawadau

MKUU MPYA WA WILAYA YA MISSENYI AAPISHWA RASMI TAYARI KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE YA KAZI KATIKA WILAYA HIYO

 Bw. Fadhili Nkurlu Mara Baada ya Kuapa Akikabidhiwa Vitendea Kazi
Mkuu  wa Wilaya ya Missenyi Bw.Fadhili Nkurlu
 Mkuu Mpya wa Wilaya ya Missenyi Bw. Fadhili Nkurlu Akiapa Mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. John Mongella
 Picha ya Pamoja
Wakuu wa Wilaya za Missenyi, Biharamulo na Bukoba Wakisikiliza Kwa Makini Dua ya Kuwaombea
Wanahabari Wakitimiza Mjukumu kwa Mkuu wa Wilaya ya Missenyi.
Mkuu wa Wilaya mpya Bw. Fadhili Nkurlu  ameapishwa rasmi kushika wadhifa wa ukuu wa wilaya katika Wilaya ya Missenyi Mkoani Kagera leo Jumanne Februari 14, 2014 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera.
Mkuu huyo mpya Bw. Fadhhil Nkurlu  aliapishwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Kagera  Mhe. John Mongella  katika hafla fupi iliyoshuhudjiwa na Wakuu wa Wilaya wanaoondoka  na wale wanaobaki mkoani Kagera pamoja na wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini.
Mara baada ya kumwapisha Mkuu mpya wa Wilaya ya Missenyi  Mkuu wa Mkoa Kagera Mhe. John Mongella aliwashukuru Wakuu wa Wlaya waliohamishwa vituo vyao vya kazi kwa kushirikiana naye kuwaletea wananchi wa mkoa wa Kagera wakati wa utumishi wao mkoani hapa.
Aidha, alitoa wito kwa Wakuu wa Wilaya ambao wamehamishiwa katika Wilaya za mkoa wa Kagera kuwa mwendo ni uleule wa kuchapa kazi na ifikapo Juni 30, 2015 lazima maabara ziwe zinafanya kazi bila kisingizio chochote.
Akimpa nasaha Mkuu Mpya wa Wilaya ya Missenyi Bw. Fadhili Nkurlu Mkuu wa Mkoa Mhe. Mongella alisema anatakiwa kuwa kama panya kuanguka huku akikimbia akimaniisha kuwa anatakiwa kujifunza huku akitekeleza majukumu yake bila kusita  kusonga mbele.
 Mkuu wa Wilaya Mpya Bw. Fadhili Nkurlu alisema yupo tayari kutekeleza wajibu wake kwa kuzingatia  taratibu, kanuni na sheria aidha, yupo tayari kujifunza kutoka kwa Wakuu wa Wilaya wakongwe na wananchi ili kuleta maendeleo kwa wananchi wa Wilaya ya Missenyi.
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Kanali Mstaafu Issa Njiku akitoa neno kwa niaba ya Wakuu wa Wilaya wenzake wanaohama mkoa wa Kagera alisema anashukuru sana kwa uongozi wa mkoa wa Kagera pamoja na wananchi kwa kuwaonesha ushirikiano mkubwa kwa kipindi walichofanya kazi Kagera.
Bw. Fadhili Nkurlu ameteuliwa kwa mara ya kwanza kushika wadhifa huo, Wakuu wa Wilaya ambao wamehamia Kagera ni kama ifuatavyo, Bw. Jackson Musome Wilaya Bukoba ametokea Musoma, Bw. Elias Tarimo Wilaya ya Biharamulo ametokea Kilosa, na Bw. Francis Mtinga Wilaya ya Muleba ametokea Chemba .
Waliobaki ni Bi Darry Rwegasira  Karagwe, Lt. Kanali Benedict Kitenga Kyerwa, na Bw. Constantine Kanyasu Ngara. Aidha Waliohama ni Bw. Richard Mbeho Kutoka Biharamulo amehamia Momba, Bw. Lembris Kipuyo kutoka Muleba kwenda Rombo, Bi  Zipporah Pangani kutoka Bukoba kwenda Igunga na Kanali Issa Njiku kutoka Missenyi kwenda Wilaya ya Mlele mkoani Katavi.

Next Post Previous Post
Bukobawadau