TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI RAIS KIKWETE ATEUA WAKUU WA WILAYA WAPYA 27
RAIS KIKWETE ATEUA WAKUU WA WILAYA
WAPYA 27
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
*Atengua uteuzi wa Ma-DC 12,
awabadilisha vituo 64, awabakiza 42 kwenye vituo vyao vya zamani
RAIS Jakaya Kikwete amefanya
mabadiliko ya Wakuu wa Wilaya kwa kuwateua Wakuu wapya 27, kuwahamisha vituo
vya kazi 64 na wengine 42 amewabakisha kwenye vituo vyao vya kazi vya zamani.
Akizungumza na waandishi wa habari
kwenye ukumbi wa OWM TAMISEMI leo mchana (Jumatano, Februari 18, 2015) Waziri
Mkuu Mizengo Pinda amesema mabadiliko hayo yamesababishwa na kuwepo kwa nafasi
wazi 27 ambazo zilitokana na wakuu wa wilaya watatu kufariki dunia; kupandishwa
cheo wakuu wa wilaya watano, kupangiwa majukumu mengine wakuu wa wilaya saba na
kutenguliwa kwa uteuzi wa wakuu wa wilaya 12.
Hata hivyo, Waziri Mkuu alisema,
Rais Kikwete amewabadilisha vituo vya kazi wakuu wa wilaya 64 na kuwabakiza
kwenye vituo vyao vya zamani wakuu wa wilaya 42.
Wakuu wa Wilaya wapya 27
walioteuliwa ni Mariam Ramadhani Mtima anayeenda Ruangwa; Dk. Jasmine B. Tiisike
anayeenda Mpwapwa; Pololeti Mgema (Nachingwea); Fadhili Nkurlu anayeenda
Misenyi; Felix Jackson Lyaniva anayeenda Rorya na Fredrick Wilfred Mwakalebela
anayeenda wilayaya Wanging’ombe.
Wengine na vituo vyao kwenye mabano
ni Zainab Rajab Mbussi (Rungwe); Francis K. Mwonga (Bahi); Kanali Kimiang’ombe
Samwel Nzoka (Kiteto), Husna Rajab Msangi (Handeni), Emmanuel J. Uhaula
(Tandahimba); Mboni Mhita (Mufindi); Hashim S. Mgandilwa (Ngorongoro); Mariam
M. Juma (Lushoto); Thea Medard Ntara (Kyela); Ahmad H. Nammohe (Mbozi); Shaban
Kissu (Kondoa) na Stephen Zelothe (Musoma).
Wengine ni Pili Moshi (Kwimba);
Mahmoud A. Kambona (Simanjiro); Glorius B. Luoga (Tarime); Zainab R. Telack
(Sengerema); Bernard Nduta (Masasi); Zuhura Mustafa Ally (Uyui); Paulo Makonda
(Kinondoni); Mwajuma Nyiruka (Misungwi) na na Maftah Ally Mohamed (Serengeti).
Wakuu wa Wilaya saba ambao uteuzi
wao umetenguliwa lakini watapangiwa kazi nyingine ni Brig. Jenerali Cosmas
Kayombo aliyekuwa Simanjiro; Kanali Ngemela E. Lubinga (aliyekuwa Mlele); Juma
S. Madaha (aliyekuwa Ludewa); Mercy E. Silla (aliyekuwa Mkuranga); Ahmed R.
Kipozi (aliyekuwa Bagamoyo); Mrisho Gambo (aliyekuwa Korogwe) na Elinas A.
Pallangyo (aliyekuwa Rombo).
Waziri Mkuu pia aliwataja Wakuu wa
Wilaya 12 ambao uteuzi wao umetenguliwa kutokana na sababu za umri, kiafya na
kuimarisha utendaji Serikaini na wilaya zao kwenye mabano kuwa ni James K. Ole
Millya (Longido); Elias Wawa Lali (Ngorongoro); Alfred Ernest Msovella
(Kongwa); Danhi Beatus Makanga (Kasulu); Fatma Losindilo Kimario (Kisarawe);
Elibariki E. Kingu (Igunga); Dk. Leticia Moses Warioba (Iringa); Evarista N.
Kalalu (Mufindi); Abihudi M. Saideya (Momba); Martha J. Umbulla (Kiteto);
Khalid J. Mandia (Babati) na Elias Goroi (Rorya).
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA.
JUMATANO, FEBRUARI 18, 201