Bukobawadau

TANGAZO LA STUDIO MPYA YA KUREKODI NA KUKUZA VIPAJI VYA WASANII NA VIKUNDI VYA KWAYA ILIYOKO KASHURA, BUKOBA MJINI

SHIRIKA LA COSAD TANZANIA, KUPITIA KITUO CHAKE CHA KUREKODI NA KUKUZA VIPAJI VYA WASANII NCHINI KIJULIKANACHO KAMA “IMUKA RECORDING STUDIOS” WANAKUTANGAZIA PROMOTION AU PUNGUZO KUBWA WEWE MSANII, KIKUNDI CHA SANAA AU KWAYA…

IMUKA RECORDING STUDIO NI STUDIO MPYA KABISA YA KISASA ILIYOFUNGULIWA MWISHONI MWA MWAKA JANA NA KUANZA KAZI ZAKE RASMI MWAKA HUU. INATUMIA VYOMBO VYA KISASA NA PRODUCERS WA KIMATAIFA KUTOKA UGANDA NA MAREKANI…

SASA UNAWEZA HUITAJI KUSAFIRI SIKU NZIMA AU KWENDA MBALI KUREKODI ALBUM YAKO….KARIBU KATIKA STUDIO ZA IMUKA ZILIZOKO KATIKA MANISAPAA YA BUKOBA UWEZE KUREKODI, KUSAIDIWA KUTAFUTIWA MASOKO AU KUFADHILI CONCERT YAKO KWA PUNGUZO KUBWA LA BEI…

 JE UNAJUA UNAWEZA KUREKODI WIMBO KWA LAKI MOJA TU AU ALBUM NZIMA CHINI YA LAKI TANO!!!
 KWA MAWASILIANO ZAIDI PIGA SIMU: 0786-024-210 AU 0757-043-750 AU 0784-425-433 AU TUMA BARUA PEPE: BUKOBA@GMAIL.COM
Kwa Wasanii na Wanakwaya Wote Mkoani Kagera na Tanzania Nzima kwa Ujumla

Kwa Wasanii na Wanakwaya Wote Mkoani Kagera na Tanzania Nzima;
  1. UTANGULIZI (INTRODUCTION AND BACKGROUND) 
Imuka Recording Studio ni kituo cha kisasa cha kurekodi na kukuza vipaji vya Kwaya na vikundi au wasanii mbalimbali nchini Tanzania na Afrika Masharki kwa ujumla kinachomirikiwa na taasisi (NGO) ijulikanayo kama COSAD Tanzania.

Kituo (Studio) imewekezwa kwa kutumia teknolojia na  vyombo vya kisasa vilivyotolewa na marafiki wa COSAD walioko Canada baada ya kuvutiwa na kusikia nyimbo zilizoimbwa na kikundi cha “Imuka Singers” kilichojumuisha waimbaji kutoka kwaya mbalimbali za Bukoba waliofanya ziara yao huko nchini Marekani mwaka 2011.

Kituo hiki kilichopo ndani ya ofisi kuu za COSAD-Tanzania  zilizopo Kashura, katika Manispaa ya Bukoba kilifunguliwa na Ugeni mzito na sherehe kubwa zilizojumuisha viongozi mashuhuri ndani na nje ya nchi wakiwemo: Mwakilishi wa Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Maaskofu Dr. Benson Bagonza, Dr. Method Kilaini, Mbuge wa Bukoba Mjini na Waziri Mstaafu  Mhe. Balozi Khamis Kagasheki na wafanyabishara na waandishi wa habari kutoka nchini kote pamoja na wasanii kutoka Dar es Salaam, Kampala na Bukoba.
  1. FAIDA ZA KUREKODI NA IMUKA (BUSINESS MODEL & COMPETITIVE ADVANTAGE) KWA MSANII AU KWAYA

  • Kukuza Vipaji na Masoko ya Muziki wa Wasanii Nje na Ndani ya Nchi: Imuka Studio ni zaidi ya sehemu ya kurekodi nyimbo zako. Ni sehemu ya kukuza vipaji na ni mdau wa wasanii kusaidia kutafuta masoko ndani na nje ya nchi kwa mfano kusaidia kuuza album yako wakati wa ziara za Kwaya ya Imuka nchini USA, au Canada au kudhamini matamasha (concerts) wakati msanii anapomaliza kurekodi na Imuka Studio.
Utaalam Uliobobea: Producer na Engineer wa Imuka Daniel Oyerwot (DJ Dan Magic) kutoka Uganda mbali na kufuzu katika vyuo vikuu vya uhandisi wa
WATU WOTE MNAKARIBISHWA!!

Next Post Previous Post
Bukobawadau