WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI KASHAI HATARINI KUKUMBWA NA MAGONJWA YA MILIPUKO
Wanafunzi wa shule ya msingi Kashai
iliyopo mjini bukoba wapo hatarini kukumbwa na maradhi mbalimbali ikiwemo
kuharisha kutokana uwepo wa Dampo ambalo lipo kandokando mwa Mto Kashai ambapo
wanafunzi hao huchota maji kila siku kwa matumizi mbalimbali ikiwemo kunywa
wakiwa shuleni.
ITV imefika katika Dampo hilo ambapo imeshuhudia wanafunzi wakichota maji
katika eneo hilo huku kukiwa na baadhi ya vinyesi mbalimbali vya binadamu
katika eneo hilo na kushuudia baadhi ya wananchi wakimwaga uchafu katika mto
huo huku wanafunzi wa shule ya msingi Kasha wakichota maji ambayo yamekuwa
yakitumika kwa matumizi mbalimbali ikwemo kunywa hali ambayo inaweza
kusababisha mlipuko wa magonjwa kwa wanafunzi hao.
Mkuu wa shule ya Msingi Kashai
Lebesi Byangwam amesema eneo hilo sasa limekuwa hatarishi kwa afya za wanafunzi
na wananchi wanaolizunguka eneo hilo kwakuwa limekuwa likichangia katika
kuchafua chanzo cha mtuo huo ambapo ameiomba serikali kufanya utaratibu wa
kuhamisha Dampo hilo haraka ili kunusuru maisha ya wafunzi wanaosoma katika
shule hiyo.
Nao baadhi ya wafanya biashara
waliopo katika soko la kashai wameonyesha kukelwa na Dampo hilo ambalo sasa
limekuwa kikwazo kwa nanchi wanaoishi katika eneo hilo nakwamba serikali isipo
chukua hatua za makusudi za kuliondoa Dampo hilo ambalo lipo kandokando mwa mto
huo wananchi wataathirika kwa kiasikikubwa napia wamechoshwa na harufu mbaya
inayotoka katika Dampo hilo hali ambayo inaweza kuhatarisha maisha ya wananchi
pamoja na wanafunzi wanaosoma katika shule ya msingi kashai.
ITV imemtafuta kaimu mkurugenzi
mtendaji wa halmashauri ya maispaa ya bukoba CHIBUNU LUKIKU bilafanikio
kwalengo la kujua kwa kina hatua zitakzo chukuliwa na serikali juu ya kusafisha
Dampo hilo na kujaribu kumtafuta kwa njia ya simu ambapo simu yake haikuweza
kupatikana.