BALOZI KAMALA AKUTANA NA MWAKILISHI WA CHAMA CHA WAFANYABIASHARA WA LUXEMBOURG
Balozi wa Tanzania Ubeligiji, Luxembourg na Jumuiya ya Ulaya Dr.
Diodorus Buberwa Kamala (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na
Mkurugenzi wa Masuala ya Kimataifa wa Chama cha Wafanyabiashara cha
Luxembourg Bwana Jean Claude Vesque. Bwana Claude alimtembelea Balozi
Kamala leo ofisini kwake Brussels. Kushoto ni Bwana Jofrey Kabakaki
afisa wa masuala ya uchumi Ubalozi wa Tanzania Ubeligi.