BARAZA LA USHAURI SUMATRA LAZINDUA VILABU VYA WANAFUNZI
Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la watumiaji wa Huduma za Usafiri wa nchi Kavu na Majini (SUMATRA CCC), Ayoob Omary akizindua vilabu vya wanafunzi vya Sumatra. Kushoto ni Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Oscar Kikoyo na kulia ni Mnadhimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Johansen Kahatan.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la watumiaji wa Huduma za Usafiri wa nchi Kavu na Majini (SUMATRA CCC), Oscar Kikoyo akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
Mnadhimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Johansen Kahatano akizungumza.
wanafunzi wakifuatilia hotuba za uzinduzi kutoka kwa viongozi.
Mgeni rasmi pamoja na meza Kuu ikipiga picha na Vilabu mbalimbali kutoka shule za sekondari na msingi.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la watumiaji wa Huduma za Usafiri wa nchi Kavu na Majini (SUMATRA CCC), Oscar Kikoyo (kulia) akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Oysterbay, Dar es Salaam jana baada ya uzinduzi wa klabu za wanafunzi watumiaji wa huduma za usafiri mkoa wa Dar es salaam jana. Wengine ni Mnadhimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Johansen Kahatano na Mwenyekiti wa Baraza hilo Ayoob Omary. Picha na Sori: mrokim.blogspot.com