FREDERICK MWAKALEBELA ASEMA JIMBO LA IRINGA MJINI MALI YA CCM 2015
Kamanda wa uvccm wilaya ya Iringa mjini Frederick Mwakalebela akiwahutubia wananchi ktk uwanja wa mwembetogwa ktk mkutano ulioandaliwa na uvccm Iringa mjini
Wananchi Iringa mjini wakiwa ktk mkutano wa uvccm Iringa mjini
kada wa CCM Bw Ahmed Mbata mwenye miwani akimzuia kijana wa CCM kuendelea kumthibiti kada wa Chadema aliyeanguka chini baada ya kupigwa kwa tuhuma za kutaka kuvuruga mkutano wa UVCCM |
Vijana wa CCM wakisogea kumshambulia kijana aliyetaka kuvuruga mkutano wao |
Wananchi wakimtazama kijana wa Chadema aliyetaka kuvuruga mkutano wa CCM |
Wananchi wakitazama tukio hilo |
Askari polisi akizuia vurugu hivyo |
Mwakalebela kushoto akiwa na katibu wa UVCCM Iringa |
Na MatukiodaimaBlog
KAMANDA wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi
(UVCCM) wilaya ya Iringa mjini Frederick Mwakalebela atuma salam kwa
upinzani jimbo la Iringa
mjini kuwa mwisho wao kuongoza jimbo
hilo ni oktoba mwaka huu hivyo wananchi
wajiandae kwa sherehe za kulipokea jimbo.
Alisema kuwa ni jambo la kushangaza kuona mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa akikodi majeshi (wanasiasa wenzake )nje ya Iringa mjini ili kusaidia mashambulizi baada ya kuona hali ya upepo kwakwe si nzuri .
" naomba kuwahakikishieni kuwa jimbo hili tulikosea mwaka 2010 ila kwa mwaka huu haturudii kosa lazima jimbo lirudi CCM"
Hivyo alisema kuwa ni ukweli usiopingika kuwa lazima Chadema wajipange kukabidhi jimbo hilo kwa Ccm na kuwa maandalizi ya kupokea yamekwisha fanyika.
Akielezea kuhusu umuhimu wa vijana kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura alisema ili Ccm uweze kushinda kuanzia udiwani ,ubunge na Urais ni lazima wakajitokeza kujiandikisha ktk daftari hilo .
Kwani alisema hakuna ushindi bila ya vijana kujitokeza kujiandikisha na kuwa iwapo kila mmoja atajiandikisha ushindi wa CCM upo wazi .
Kwa upande wake katibu wa CCM mkoa wa Iringa Hassan Mtenga akihutubia wananchi hao alisema kuwa mbunge msigwa anapaswa kujiandaa kisaikolojia kwani CCM imejipanga vema kuona jimbo hilo linarudi mikononi mwa CCM kwa mwaka huu .
Alisema kuwa jimbo hilo CCM kililianzimisha kwa Chadema hivyo muda wao wa kuendelea kulikalia umepitwa kutokana na mbunge kushindwa kuwatumikia vema wananchi wa jimbo hilo wakiwemo vijana ambao waliahidiwa ajira ila hadi leo vijana Iringa mjini wamegeuka omba omba kutokana na kutokuwa na ajira .
Hivyo alisema mbali ya mbunge wa sasa muda wake kumalizika bado anapaswa kuwaeleza wananchi wa jimbo la Iringa mjini matumizi ya fedha za mfuko wa jimbo ambazo amekuwa akizipata zimefanya kazi gani katika jimbo hilo lasivyo CCM itakuja na orodha kamili ya ahadi zake na kiwango halisi cha fedha za mfuko wa jimbo .
Mtenga alisema Chadema imekuwa ikiendesha siasa za vurugu kwa kuwatumia vijana kuvamia mikutano wa CCM hasa pale wanapoona wananchi wamejitokeza kwa wingi kwa lengo la kutaka kuivuruga na kuwa kuanzia sasa CCM inawaomba vijana hao kuacha kutumika kwa mashali ya wachache na kuwa iwapo watashindwa uvumilivu wa sera za CCM ni vema wasifike katika katika mikutano badala ya kufika kwa lengo la kufanya fujo.