JK ASIKITISHWA NA MATAMKO YA VIONGOZI WA DINI YA KUWATAKA WAUMINI KUPIGA KURA YA HAPANA KATIBA PENDEKEZWA
Rais Jakaya Kikwete amesema
amesikitishwa na kushangazwa kwa kitendo cha baadhi ya viongozi wa dini
kutoa matamko kwa waumini wao ya kuwataka kupiga kura ya hapana kwa
katiba inayopendekezwa na kuongeza kuwa hakuwahi kudhani wala
kufikiri kuwa kwa viongozi aliowaheshimu kama wangeweza Kufanya jambo
kama hilo kwa waumini wao.
Mh.Kikwete ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na viongozi wa dini
kupitia kamati ya amani ya mkoa wa Dar es Salaam ambapo amesema kitendo
walichofanya viongozi hao wa dini kingeweza kuwa na tija kama katiba
inayopendekezwa ingekuwa inawanyima uhuru wa kuabudu.
Na kuhusu mahakama ya kadhi Mh.Kikwete amesema serikali haitaanzisha ila waislamu wenyewe wana uhuru wa kuwa nayo amala.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh.Said Meck Sadick
amesema uwepo wa hali ya utulivu hasa katika mkoa wa Dar es Saam
imewezekana kutokana na viongozi wa Dini kuwa naumoja ambao kila
mara wamekuwa mstari wa mbele kusaidia amani idumu nchini.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati hiyo Sheikh mkuu wa mkoa wa
Dar es Salaam Alihadi Mussa Salum amesema mkutano huo unalengo la
kujadili mambo makubwa yanayolihusu taifa ambapo makamu Mwenyekiti
wa kamati hiyo askofu Valentino Mokiwa amesema bado ipo
changamoto ya matumizi ya Demokrasia iliyopo nchini.