MADEREVA 21 WA KAMPUNI YA MAJINJAH LOGISTICS LTD WAPATIWA MAFUNZO CHUO CHA TAIFA CHA USAFIRISHAJI (NIT) WAHITIMU WAPEWA VYETI.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Majinjah Logistics Ltd wakiwa katika picha ya pamoja na kutoka kushoto mstari wa mbele (wa pili) Mkuu wa Kampuni ya Majinjah,Geoffrey Mwambona, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Majinjah Logistics,Benjamin Mwandete,Mkuu wa Idara ya Tafiti,Machapisho na Masomo ya Elimu ya Juu (NIT),Dk,Ethel Kasembe,Mhandisi, Charles Kisunga na Dereva wa kike wa Majinjah,Grace Andrew.
Wahitimu wa mafunzo ya Udereva wa Kampuni ya Majinjah Logistics wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wao na viongozi wa NIT.
Mhandisi, Charles Kisunga wa NIT akizungumza,Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Majinjah Logistics,Benjamin Mwandete (kushoto) Mkuu wa Idara ya Tafiti,Machapisho na Masomo ya Elimu ya Juu (NIT),Dk,Ethel Kasembe (wa pili kulia) na Mkuu wa Kampuni ya Majinjah,Geoffrey Mwambona,
Mkuu wa Idara ya Tafiti,Machapisho na Masomo ya Elimu ya Juu,Dk,Ethel Kasembe (kulia) akizungumza kabla ya kukabidhi vyeti wahitimu.Wengine ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Majinjah Logistics,Benjamin Mwandete na Mhandisi, Charles Kisunga wa NIT.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Majinjah Logistics,Benjamin Mwandete (kushoto) akitoa nasaha kwa wahitimu.
Mwalimu wa Madereva, Daniel Kasisi,akifuatilia utoaji wa Vyeti kwa Wahitimu 21 wa Maginjah Logistics Ltd.
Na Mwandishi Wetu
Madereva 21 wa Kampuni ya Majinjah Logistics Ltd wamepatiwa mafunzo ya siku tatu katika Chuo cha Taifa cha Usafirishji (NIT).
Mafunzo hayo yalihusu Alama na Michoro ya barabarani,Sheria,Udereva wa Kujihami,Vyanzo vya Ajali jinsi ya kuzizuia,Huduma kwa Wateja na mawasiliano ya Barabarani.
Mkuu wa Idara ya Tafiti,Machapisho na Masomo ya Elimu ya Juu,Dk,Ethel Kasembe,aliwaambia madereva kuwa elimu waliyoipata itawasaidia kuepusha ajali za barabarani wakati wakiendesha mabasi yanayobeba abiria na kuwataka waendelee kupata elimu ya kutosha.
Alisema kuwa imani yake takwimu za ajali zitapungua na hata kwisha kabisa kama watazingatia waliyofundishwa na kuwasisitiza kwenda Chuoni hapo mara kwa mara kuendelea kupata elimu.
Pia alisisitiza kuwa watabadilika baada ya kumaliza mafunzo ya hapo na kuwa vyanzo vya ajali watavizuia kwa kutumia udereva wa kujihami wakiwa barabarani wakati wote.