MJUWE SHABANI GURUMO 'MNIKULU'
Majukumu yake kama Mnikulu na maelezo ya Utangulizi
Kazi yake kubwa ni kusimamia majengo yote ya ikulu kwa maana ya shughuli za utawala. Yeye ndiye anahusika na usafi na decorations zote zinazohusu ikulu. Ni mtu anayeweza kuamua muonekano wa ikulu ukoje na hata kupanga na kuamua aina ya nguo, mashuka, mapazia n.k. yanayopaswa kutumiwa na rais. Kwa majukumu haya, anapaswa amjue vizuri rais wake.CHANZO:JF
Kwa kuzingatia majukumu yake na tabia yake ya kifisadi kama itakavyofafanuliwa vizuri hapo baadaye, Shabani ameingiza serikali kwenye mikataba isiyo na tija ya kununua mapazia na furniture za bei mbaya kutoka nje ya nchi.
Unajua, ikulu inapaswa kuwa ni pride ya nchi; ni aibu na ajabu kwa Tanzania kununua furniture kutoka Afrika Kusini ambazo zinaweza kutengenezwa na Magereza au JKT au hata vijana wa Keko. Tena furniture za hapa zinatumia mbao imara kuliko hizo wanazonunua kutoka Afrika Kusini na Uarabuni. Kwa kudokezea tu, naweka ushahidi wa manunuzi aliyofanya huyu jamaa ya mapazia na hizo furniture.
Siyo kwamba Rais Kikwete hajui, he knows everything and he is indirectly and directly benefiting from Shabani’s activities.
Shabani amefanikiwa kukusanya fedha nyingi sana kutoka katika ufisadi huu na kupitia kwenye biashara zake zinazofanikiwa kwa mgongo wa ikulu na ukaribu wake na rais. Katika aya zinazofuata ntafafanua hili kwa undani.
Connections with JK and family
Wafuatiliaji wa mambo wanasema mama yake Rais Kikwete alifariki wakati Rais Kikwete ni mdogo sana. Hivyo Rais Kikwete akalelewa na mama yake Shabani. Huu ndiyo undugu uliopo. Infact, Shabani ni sehemu ya familia ya Rais Kikwete. Ni mtu wake wa karibu kwa masuala ya kikazi na kibinafsi. Anahusika pia hata kuwahudumia wale wachawi wake wanaotembelea ikulu mara kwa mara.
Ukiwa unafanya kazi ikulu na ukitaka kibarua chako kiote nyasi, korofishana na Shabani. Nakumbuka wakati fulani, Shabani ndiye alikuwa analetwa OBR ili achukue nafasi ya Jairo kama Katibu wa Rais, kwa bahati, baadhi ya wazee walipinga sana.
Shabani huwa anahakikisha anapigana na kufanikisha shughuli zote za kibiashara na kisiasa zinazowahusu watoto wa Rais Kikwete. Vijana wangu walifanikiwa kukamata simu yake ya mkononi wakati fulani na kukuta kwenye phonebook yake kuna contacts zote za wafanyakazi wa ile kampuni ya Lugumi Enterprises Ltd – Kampuni inayonunua vifaa vya kijasusi na vya kijeshi kwa niaba ya vyombo vyetu vya dola kana kwamba vyombo vyetu haviwezi kununua vyenyewe moja kwa moja. Utakumbuka ushiriki wa Ridhiwani kwenye kampuni hii na michezo yao yote hasa wakati wa Gen. Shimbo.
Biashara anazofanya akiwa Ikulu
Unajua ingawa Rais Kikwete alisema haendi Ikulu kufanya biashara, kauli yake inatofautiana na facts on the ground. Watu wake wanaomzunguka wanajihusisha na biashara tena wakiwa hapo hapo ikulu; yeye anajua na usalama wa taifa wanajua vizuri sana.
Mfano huyu Shabani anahusika moja kwa moja na yuko busy sana na biashara / makampuni haya yafuatayo:
- Fitness Master (T) Ltd akiwa na 15% share.
- Wenzake alionao ni pamoja na raia wa Denmark anayeitwa Jorgen Hyldahl na jamaa mmoja anayekaa UAE anayeitwa Abdulhamid Mhona.
- Kampuni yao inamiliki Centers katika majiji ya Dar, Arusha na Mwanza.
- Masagalu Gold Mining Company akiwa na 25% share. Wenzake alionao ni Najim Zuberi Msenga 65% na Ahmed Salim Masood 15%
Shabani amekuwa akisumbuliwa sana na upatikanaji wa gesi iliyogunduliwa Mtwara. Ameamua kununua eneo, akishirikiana na Mhona kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya ofisi ili ayapangishe makampuni ya uchimbaji gesi na madini. Tayari ana hakikisho la kupata wapangaji Seven Anchor Property and Services, kampuni anayoonekana kuimiliki kwa sehemu kubwa yeye mwenyewe.
Hawa Seven Anchor watafilisi nchi muda si mwingi. Wanaingia michezo michafu sana ya kujitwalia majengo kwa kushirikiana na NSSF wakitumia staili kama ile ya Quality Plaza ambayo kipindi kile iliripotiwa sana na gazeti letu pendwa la ThisDay. Kwenye dossier ya pili itakayokuwa na viambatisho tutaweka ushahidi wa mauziano (receipt) na mikataba waliyosainishiana na NSSF kwa msaada mkubwa wa Dr. Dau.
Shabani’s Business Intrigues
Connections with Yussuf Manji (Fisadi Papa):
Shabani na Manji ni wasiri wakubwa sana. Shabani amefikia kuwa kama speech writer wa Manji. Nakumbuka kuna barua moja ambayo Manji alitaka kumuandikia rais kuhusu masuala ya Yanga.
Ni Shabani ndiye alii draft na kumpatia Manji ili aisaini. Hapa nitaweka ushaidi mwingi wa kimawasiliano kati yao hatua kwa hatua endapo yeye au mtu yeyote atajitokeza kubisha. Ushahidi umekusanywa kupitia simu na njia nyingine nyingi.
Manji na Shabani wanashirikiana sana katika kufanya serikali ikubali na kupitisha miradi ya Manji hata kama taratibu za PPRA hazifuatwi. Ni Manji ambaye humpa mbinu Shabani za namna gani taratibu za PPRA zikiukwe; ushahidi upo kwenye sakata la Tender No PA/001/12/HQ/G/001 Closing Date 12th October, 2012 inayohusu Supply of ABC Cables, Conductors and its Accessories hii ni mradi wenye thamani USD 60.0 million. Ni fedha nyingi sana.
Mradi mwingine ni ule wenye thamani ya usd 35 milioni kupitia Tender No PA/001/12/HQ/ G/002 unohusu Supply of Meters, HT Metering Units and LV Metering Cabinets. Miradi yote hii inawahusu Manji na Shabani kwa asilimia 100%. Habari nilizonazo, tayari Shabani ameanza kuchezesha huu mchezo pale tanesco.
Mradi mwingine ambao Shabani ameelekezwa na Manji ni ule Tanzania Oil and Gas Investments. Mchezo waliucheza kwa kushirikiana na bosi wa TPDC. Katika eneo la nishati na madini, hapa wanataka kuingia ndani sana na ndiyo maana wakasajili ile kampuni. Ushahidi uliwekwa hapa unaelezea kidaga ubaga.
Wataanzisha miradi mikubwa mikubwa kama ya ethanol, methanol n.k. n.k. Wataanzisha miradi ya utengenezaji TV. Shabani anakuwa ni kiungo muhimu sana kwa Manji na wakubwa wengine…
Licha ya Manji, Shabani anatumika vizuri sana wafanyabiashara wengine kama Jack Gotham na Almasi Maige. Bw. Gotham ni kiungo chake kwenye ule mradi wa national Ids na Bw. Maige ni kiungo chake na kampuni ya General Electric ya Marekani ambayo inafukuzia mradi wa umeme wa NSSF. Habari nyingine zinaniambia kwamba kuna mikataba hewa ambayo Shabani ameifanikisha kati ya Ikulu na Maige na kuwa hawa jamaa hulipwa kila mwaka bila kazi yoyote. Undani wa mahusiano yake na hawa jamaa unakamilishwa.
Extra notes
Kwa sababu simu ya huyu bwana Shabani iko kwenye miliki yetu, muda si mwingi utapata mawasiliano yake hasa na watu ambao wanaonekana wako kwenye system nyeti. Kwa haraka nimeona majina ya kina Kapongwa na Zoka na maafisa usalama wengine wengi ambayo yameanza kujitokeza kwenye hii michezo hivi karibuni.
Huyu ndiye Shabani Rajab Gurumo. Hii dossier ni hatua ya mwanzo katika kuumbua uozo unaofanywa na kichwa cha serikali ya ccm. Ni hatua muhimu katika kurejesha uwajibikaji unaostahili kufanywa na viongozi wa nchi.