MWANAMUZIKI ALLY CHOKI KUTUMBUIZA TOKYO JUMAMOSI 21 MARCH 2015
Mwanamuziki mahili wa muziki wa dansi Ally Choki ambaye pia ni
kiongozi wa bendi ya Extra Bongo aka "Wazee wa Kizigo" anatarajiwa
kutingisha jukwaa siku ya Jumamosi 21.Machi 2015 ambapo wanamuziki wa
Eagle's Vission watakuwepo kumsindikiza Ally Choki anayefuatana na Super
Nyamwela.Katika onyesho hilo
wakongwe wawili wa muziki wa dansi watanzania wanaoishi Japan wanamuziki
Fresh Jumbe Mkuu na Abbu Omary watakuwepo jukwaani kuwapa baraka zote
wadogo zao Ally Choki na Super Nyamwela katika ukumbi wa Sehemu inaitwa Sonudai-Kanagawa Prefecture, Sagamihara City pembeni kiduchu ya Jiji la Tokyo.
Ally Choki na Super Nyamwela wakiwa JapanMkongwe Abbu Omary aliekuwa Simba wa Nyika
Madhumuni ya ziara ya Ally Choki na Super Nyamwela ni kuangalia ushirikiano na
uwezekano wa soko la muziki wa dansi wa Tanzania "Bongo Dansi" ili
muziki huo uweze kushika kasi kubwa na soko Japan na mashariki ya mbali
kwa ujumla,Pia
uwezekano wa bendi ya Extra Bongo kufanya ziara za kimataifa. Wadau msikose
kujitokeza kwa wingi katika Onyesho hili waswahili usema 'Chereko Chereko na mwenye mwana"
Ukumbi: Sonudai-Kanagawa Prefecture, Sagamihara City,