NGUVUNI KWA KUFUKUA KABURI LA ALBINO NA KUMNYOFOA VIUNGO WILAYANI KARAGWE!
JESHI la Polisi mkoani Kagera, linawashikilia watu wawili wakituhumiwa kufukua kaburi la marehemu Baltazar John mwenye ulemavu wa ngozi (albino) na kuchukua viungo viungo vyake. Anaandika Mwandishi wetu … (endelea).
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Henry Mwaibmbe, tukio hilo limetokea 27 Machi mwaka huu, ambapo watuhumiwa walinaswa katika nyumba ya kulala wageni ya Ford iliyopo eneo la Kyaka wilayani Missenyi.

Watuhumiwa hao ni Laston Faustine (41) mkazi wa Lukulaijo na January Korongo (43) mkazi wa Kadengesho – wote wa wilayani Karagwe, ambapo walikutwa na mifupa mitatu ya binadamu.
Kamanda Mwaibambe amesema “katika mahojiano mtuhumiwa wa kwanza- Faustine, alituambia kuwa alipewa viungo hivyo na Korongo kwa ajili ya kuviuza Sh. 20 milioni.”
Ameongeza kuwa, Korongo alipohojiwa amekiri kwamba alifukua kaburi la mjomba wake aitwae Baltazari John (albino), ambaye alifariki mwaka 1991 na mwili wake kufukuliwa 2009.
“Baada ya kumuhoji zaidi mtuhumiwa huyo, alikubali kuongozana na polisi hadi nyumbani kwake ambapo alionyesha fuvu la kichwa, mifupa mitatu ya miguu pamoja na mifupa ya sehemu mbalimbali ambayo ilikuwa imefungwa kwenye mfuko nje ya nyumba yake.
“Ili kujiridhisha, jeshi liliomba kibali cha mahakama wilayani Karagwe ili kufukua kaburi hilo kuhakikisha kama kweli kuna mabaki ya mwili huo. Tulipofukua hakuna kilichopatikana,” amesema kamanda.