NONDO KWA JUMATANO YA LEO MARCH 18,2015
Watoto kwenye ndoa sio chanzo cha furaha, na wala hawaji kuleta furaha
bali wanakuja kuongeza na kuendeleza furaha iliyokuwepo baina yenu ninyi
wapenzi. Ukiona mtu anasema watoto wameleta furaha maana yake haikuwepo
awali. Watoto hawawezi hata sikumoja kuchukua "kureplace" nafasi ya
furaha ya ndoa, ndoa inafuraha yake na watoto wanafuraha yao, vyote hivi
vinaleta ukamilifu wa furaha ya kweli. Inauma sana pale furaha ya ndoa
inapokufa na mtu anabaki tu kwa ajili ya watoto, inasumbua moyo sana
pale mtu anapoona hapati tena furaha kutoka kwa mume au mke wake na
anaamua kuhamishia mapenzi kwa watoto. Utamu wa asali ni wa asali na
utamu wa sukari ni wa sukari ingawa vyote ni vitamu na vyote hutumika
kwenye chai, kimoja kimetoka kwenye mmea na kingine kwenge mdudu.
Jifunze kutofautisha na kuiheshimu tofauti iliyopo.
Mara nyingine kwenye mahusiano mmoja anaweza kuamua kuanzisha mazingira ya ugomvi ili tu hali ya hewa ichafuke yeye apate upenyo wa kutoka na kwenda kwenye mchepuko au kwenye mishemishe nyingine. Kikawaida ni ngumu kuamua kuondoka kwenda kumsaliti unayempenda wakati anakuchekea na kila kitu baina yenu kiko sawa, hii inaitwa "guilty conscious" ingawa wako ambao hawana hiki kitu na wanaweza kukusaliti katikati ya kipidi cha amani na furaha tele. Sasa wengi hutumia mbinu inaitwa "chafua hewa utoke", yamkini hata haendi kwa mwanamke bali anaenda kwa marafiki zake au kwenye kinywaji na anajua wewe ni kipingamizi cha kutoka kwake basi anaamua kuchafua hali ya hewa ili asepe. Sasa basi maranyingine ukiona mwenzako anakuvuruga mivurugo isiyo na sababu kabla ya kumuuliza "kwanini unafanya hivi ?", muulize " unataka kwenda wapi?" - Chris Mauki