LISSU ATANGAZA RASMI ZITTO KUVULIWA UANACHAMA CHADEMA
Mwanasheria mkuu wa chama cha CHADEMA Tundu Lissu ametangaza kuvuliwa
rasmi uanachama kwa mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe baada ya
Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam kutupilia mbali
pingamizi la mbunge huyo la kuzuia asijadiliwe.
"Kwa mujibu wa katiba ya chama cha CHADEMA, mwanachama yoyote anapofungua kesi mahakamani dhidi ya chama chake, endapo atashindwa katika kesi hiyo atakuwa amejiondoa uanachama wake, kwahiyo natangaza rasmi rasmi Zitto Kabwe sio mwanachama tena wa CHADEMA.
Hii ni kwa kujibu wa tweet ya East Africa Radio

Wakati tukiendelea kusubiri taarifa kamili, hiki ndicho alichokisema mwanasheria wa Zitto Kabwe.
Kupitia taarifa zilizosambaa kuhusu kufukuzwa kwa Zitto Kambwe
uanachama CHADEMA, mwanasheria wake Albert Msando kaandika kupitia
Instagram taarifa hii..
Taarifa kuhusu maamuzi ya Mahakama Kuu leo tumezipata kupitia mitandao
ya kijamii kwa sababu kesi awali ilikuwa imepangwa tarehe 12.03.2015
lakini inaonekana kwenye rekodi imerudishwa nyuma na maamuzi hayo
kusomwa leo bila sisi kuwa na taarifa. Tunafanya utaratibu tupate nakala
ya maamuzi hayo ili kujua nini cha kufanya. Hatuna taarifa rasmi ya
kufukuzwa Mh. Zitto Kabwe uanachama. Taratibu zote zitafuatwa pindi
tukipokea taarifa rasmi kutoka mahakamani na kwenye chama. Ni matumaini
yetu jambo hili halitaendeleza chuki zisizokuwa na sababu au kujenga
kati ya wahusika. #Demokrasia #Haki #UtawalaBora #Taratibu