ZITTO KABWE BUNGENI LEO
Siku moja baada ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Anna Makinda kusema kuwa Zitto Kabwe ni mbunge halali wa jimbo la Kigoma
Kaskazini kutokana na ofisi yake kutokuwa na taarifa rasmi ya
kutenguliwa ubunge wake, mbunge huyo leo amehudhuria mkutano wa bunge
unaoendelea mkoani Dodoma.
Katika siku hiyo ya kwanza ya kuhudhuria bungeni hapo mara baada ya
chama cha Demokrasia na Maendeleo -CHADEMA ambacho alikuwa mbunge
kupitia chama hicho kumfukuza uanachama Mhe.Zitto Kabwe amelalamikia
hatua ya Serikali kutowatendea haki wakazi wa Kilwa kwa kutowanufaisha
na gesi inayopatikana eneo hilo.
Katika kikao hicho Zitto Kabwe amesema kumekuwa na malimbikizo ya
fedha ambazo kampuni inayohusika na kuchimba gesi katika eneo la
Songosongo Wilayani Kilwa ilitakiwa kulipa kwa halmashauri ya wilaya ya
Kilwa lakini tangu kuanza kwa uchimbaji huo kampuini husika haijalipa
fedha hizo.
Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa nishati na madini Charles
Kitwanga ameliambia bunge kuwa tayari Serikaliimegundua madhaifu hayo na
kwamba kwa sasa ipo katika mchakato wa kutathmini halmashauri hiyo
inadai shilingi ngapi na hatimaye iweze kulipwa.