Bukobawadau

CAMERA YETU SHULE YA MSINGI BUHORORO WILAYANI NGARA

 Wananfunzi wa shule ya msingi Buhororo wilayani Ngara mkoani Kagera wakiwa katika shughuli za kupanda maua shuleni hapo katika mipango mikakati ya kulinda na kuhifadhi Mazingira
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Buhororo Wilayani Ngara  wakifanya usafi katika mazingira ya shule yao kabla ya kuingia madarasani .
 Baada ya shughuli za kuhifadhi mazingira walimu huingia madarasani na kufundisha masomo yao kama wanavyo onekana pichani wakipitia kazi za wanafunzi
Walimu  wa Shule ya Msingi Buhororo pichani ni Mwl.Happy Mshumbuzi na Peter Charles wakiendelea kuzipitia kazi za wanafunzi na kusahihisha
Walimu wa Shule ya Msingi Buhororo wameanzisha utaratibu wa kula shuleni hapo kila mchana  hii ni pamoja na wanafunzi
 Hii ni baada ya kuondoa ule utaratibu wa ikifika mchana waende kula nyumbani na kurejea  tena mpaka jioni.
  Baadhi ya Walimu katika utaratibu wa kupata chakula cha mchana.
Wanaonekana sehemu ya Wanafunzi shuleni hapo mara baada ya kupata Chakula ,wakiwa tayari kuendelea na masomo yao mpaka jioni ,huu ni utaratibu unaopelekea wanafunzi  kufanya vizuri kitaaluma. Picha na  Shaaban Ndyamukama


Next Post Previous Post
Bukobawadau