HABARI KUTOKA ITV
HABARI ITV:Hali ya taharuki imewapata wakazi wa kijiji cha Park Nyigoti
kata ya ikoma wilaya ya Serengeti baada ya mahakama kutoa ruhusa ya
kufukuliwa kwa mwili wa Bi. Celina Jumapili aliyefariki dunia na kuzikwa
tarehe tatu marchi kisha kuonekana utata katika kaburi lake ambalo leo
limefukuliwa na kukuta sehemu ya viungovya mwili wake vimekatwa vikiwemo
kiganja cha mguu vidole vya mkono wa kushoto na sehemu za siri zikiwa
zimenyofolewa hali iliyozua mashaka makubwa kwa wakazi wa kijiji hicho