KUHUSU WATU 9 KUKAMATWA NA SILAHA MSIKITINI MOROGORO
HABARI ZAIDI Kuhusu Watu 9 Wakamatwa Msikitini na Silaha, Milipuko, Majambia na Bendera ya Al Shaabab Morogoro
Jeshi la polisi mkoani Morogoro limekamata watu 9 wakiwa na silaha za kulipua na nguo za jeshi la wananchi wakiwa wamejifungia katika msikiti wa Suni Kidatu wilayani Kilombero mkoani Morogoro.
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paul amesema tukio la kukamatwa kwa watu hao limekuja kufuatia jeshi la polisi kupata taarifa za uhalifu ambapo jambazi mmoja aliruka katika bajaji na kisha kumjeruhi askari shingoni ambapo wananchi wenye hasira kali walioshuhudia tukio hilo walimkimbiza jambazi huyo akiwa na silaha na kisha kumchoma .
Kamanda Paul amesema kufuatia tukio hilo jeshi la polisi liliongeza nguvu ya askari ambapo walifanya msako mkali na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wengine wakiwa katika msikiti wa Suni Kidatu na baada ya kupekuliwa wamekutwa na vifaa vya milipuko nguo za kijeshi la wananchi wanaendelea kuwashikilia watuhumiwa na kuna taarifa kuwa watuhumiwa hao walijiandaa kufanya tukio la uhalifu .

Aidha kamanda paul amewashukuru wananchi wa ruhembe kidatu wilayani
kilomeroa mbao wametoa ushikiano kufanikisha kukamtw akwa watuhumiwa
hao.