MAUAJI YA KUKATA KOLOMEO :WATU SITA WASHIKILIWA NA POLISI MKOA KAGERA
Jeshi la Polisi mkoani Kagera limewatia mbaloni watu sita akiwemo na
mganga wa kienyeji moja anaedaiwa kufadhili vitendo vya mauaji ya
kunchinja watu na kuondoa badhi ya viungo na wengine wawili kupigwa
lisasi hadi kufa walipokuwa wakijalibukutoka mikononi mwa polisi.
Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa jeshi la polisi
mkoani Kagera ACP Henry Mwaibambe amesema jeshi la polisi sasa
linandelea na msako mkali ambapo ameongeza kuwa sasa limebaini mtandao
wa watu hao wanaojihusisha na matukio hayo nakufanikiwa kukamata watu
sita pamoja na mganga wa jadi mmoja anaedaiwa kuwafadhili watu hao
kwa kuwapa tunguli na irizi iliwaweze kufanya matukio hayo ya kinyama
nakwamba kati ya watuhimiwa hao sita wawili wamefariki dunia kwa kupigwa
risasi akiwemo kinara wa mauaji hayo wakati wakijaribu kutoroka mikono
mwa polisi.