MISUGUANO NDANI YA NDOA !
Matatizo na misuguano mingi ndani ya ndoa husababishwa na mwanandoa
mmoja au wote kutaka kuishi maisha kama bado yuko "single" hajaoa au
hajaolewa wakati tayari yuko kwenye ndoa, kama ulikuwa hujatosheka na
maisha yako ya u single nini kilikufanya ukimbilie kwenye ndoa??? Au
ulikuwa unatafuta kuosha nyota tu??? Sasa angalia umeingia kwenye ndoa
na bado hamuishi kuminyana na kukwaruzana mwishoni mtatoana roho.
Sikiliza nikwambie ukweli, kama umeamua kuoa au kuolewa, au kama umeamua
kuingia kwenye ndoa, waza kama mwanandoa, zungumza kama mwanandoa,
tenda kama mwanandoa na ishi kama mwanandoa, nothing more nothing less,
utoto waachie watoto