Bukobawadau

MKUCHIKA:AKIRI TAIFA LINAKABILIWA NA MPOROMOKO WA MAADILI KWA VIONGOZI WA UMMA

Waziri wa nchi ofisi ya rais utawala bora Capteni George Mkuchika amekiri kuwa taifa linakabiliwa na mporomoko mkubwa wa maadili kwa viongozi wa umma  tatizo ambalo amedai linaigharimu taifa katika nyanja zote ikiwemo siasa, kiuchumi na kijamii.
Capteni mkuchika ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na wadau wa maadili waliokuwa wanajadili rasimu ya mwongozo wa maadili ya viongozi wa umma ambapo amesema athari ya ukiukwaji wa maadili na mgongano wa maslahi ni kubwa na madhara yake yanaweza kuligharimu taifa na kudhohofisha maendeleo ya nchi na kwamba tatizo hilo limeongezeka baada ya utaratibu wa vijana kujiunga na jeshi la kujenga taifa kufutwa.

Baadhi ya viongozi walioshiriki wakiwemo wanasiasa wameshauri TAKUKURU kupewa nafasi ya kumalizia kazi wanazochunguza kwa kuzipeleka mahakamani moja kwa moja badala ya kupitia kwa mkurugenzi wa mashitaka ili kupunguza tatizo la rushwa hapa nchini ambalo linapelekea taifa kwendelea kubaki maskini huku baadhi ya watu wachache wakineemeka.

Katibu wa Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma Bw.Tickson Nzunda amesema mwongozo wa maadili ya viongozi wa umma ambao unajadiliwa utakuwa mwanzo wa kampeni ya kitaifa ya kukuza maadili nchini na utatumika kama nyenzo kwenye maeneo ya kuzingatiwa na wadau wote katika utekelezaji wa majukumu yao na utadhibiti mgongano wa maslahi nchini.
ITV.
Next Post Previous Post
Bukobawadau