MTWARA YAPATA MKAKATI WA MAWASILIANO WA KUKABILIANA NA MAAFA
Mkurugenzi wa Idara ya
Uratibu shughuli za Maafa ofisi ya Waziri Mkuu, Brig.Jen. Mubazi Msuya (wa pili
kulia) akifuatilia majadiliano wakati wa uwasilishaji wa Mkakati wa Mawasiliano
wa kukabiliana na maafa kwa mkoa wa Mtwara tarehe 23 Aprili, 2015, kulia kwake
ni Katibu Tawala Msaidizi (Uchumi na Uzalishaji) Mkoani Mtwara, Bw. Johansen Bukwari.
Baadhi ya washiriki wa warsha ya uwasilishaji wa Mkakati wa Mawasiliano wa kukabiliana na maafa kwa mkoa wa Mtwara wakifuatilia uwasilishwaji wa mkakati huo, uliofanywa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu wa Shughuli za Maafa mkoani Mtwara tarehe 23 Aprili, 2015.
Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu shughuli za Maafa ofisi ya Waziri Mkuu, Brig.Jen. Mubazi Msuya (Walio kaa wa pili kushoto) akiwa na washiriki wa warsha ya Kuwasilisha Mkakati wa Mawasiliano wa kukabiliana na maafa kwa mkoa wa Mtwara mara baada ya kuwasilisha mkakati huo tarehe 23 Aprili, 2015, wa kwanza kulia kwake ni Katibu Tawala Msaidizi (Uchumi na Uzalishaji) Mkoani Mtwara, Bw. Johansen Bukwari.

Mtwara
yapata Mkakati wa Mawasiliano wa Kukabiliana na Maafa
Ofisi ya waziri Mkuu kupitia
Idara ya Uratibu wa Shughuli za maafa imewasilisha Mkakati wa Mawasiliano wa
kukabiliana na maafa kwa mkoa wa Mtwara. Mkakati huo umetayarishwa kwa ajili ya
kuhakikisha kwamba kunakuwa na Mtiririko unaoeleweka wa taarifa za tahadhari
kabla ya maafa, wakati wa maafa na baada ya maafa kutokea.
Mkakati huo umezingatia
majanga ambayo yamekuwa yakitokea mara kwa mara na kusababisha madhara makubwa
mkoani Mtwara. Majanga hayo ni; Ukame, mafuriko na mlipuko wa kipindupindu.
Akizungumza wakati wa warsha
ya kuwasilisha mkakati huo maafa mkoani Mtwara tarehe 23 Aprili, 2015, Katibu
Tawala Msaidizi (Uchumi na Uzalishaji) Mkoani Mtwara, Bw. Johansen Bukwari alifafanu kuwa mkakati
huo utaongeza nguvu ya jamii kuwa na
utayari wa kukabiliana na majanga yanayowakabili ili kuokoa maisha na
mali zao.
Bukwari, “Halmashauri za
Mtwara Mikindani na Vijijini zimekuwa na tatizo la kukumbwa na mafuriko, ukame
na magonjwa ya mlipuko mara kwa mara kutokana na mabadiliko ya tabia nchi,
ujenzi katika maeneo hatarishi pamoja na miundombinu duni, kupitia mkakati huu
kila mmoja wetu kwa kuzingatia nafasi aliyonayo ataweza kutekeleza wajibu wake
kwa ufanisi.”
Awali akimkaribisha Katibu
Tawala katika warsha hiyo, Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa shughuli za Maafa,
Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig.Jen. Mubazi Msuya alieleza kuwa uwepo wa mkakati huo
mkoani Mtwara unawezesha ufanisi wa hatua zilizokuwa zinachukuliwa na serikali mkoani
humo za kukabiliana na maafa.
“Serikali imekuwa ikichukua
hatua mbalimbali za kuhakikisha madhara yaliyotokea mkoani Mtwara hayajirudii
ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kuhusu athari za ujenzi na kuendesha shughuli za
uchumi katika maeneo hatarishi, umuhimu wa usafi wa mazingira matumizi ya mbegu
zinazostahimili ukame pamoja na kuzuia ujenzi katika maeneo hatarishi” alisema
Msuya.