PROF TIBAIJUKA ADHAMINI MAFUNZO YA WAENDESHA PIKIPIKI WILAYANI MULEBA
Waendesha pikipiki maarufu bodaboda kutoka jimbo la Muleba
kusini wakiwa kwenye mafunzo ya sheria za usalama barabarani chini ya
ufadhili wa Mbunge wa Jimbo hilo Profesa Anna Tibaijuka na kuendeshwa na Chuo cha udereva cha Lake zone
Driving School mkoani kagera na kikosi cha usalama barabarani mkoani
humo.
Mkuu wa wilaya ya Muleba Francis Isaka amewataka vijana
hao kuhakikisha wanazijua sheria na kuepuka ajali zinazogharimu maisha ya
watu na wengine kuwa walemavu wa kudumu na kupungua nguvu kazi ya Taifa.
Aidha
Mkurugenzi wa Lae zone Driving School mkoani Kagera Winstoni Kabantega
amewaasa vijana hao kuhakikisha wanaendesha vyombo vya moto wakiwa na
leseni zenye majina m halali huku wakijihadhari na ulevi mwendo kasi na
kubeba abiria zaidi ya wa chombo husika
Jumla ya vijana 411
wamejitokeza kupata mafunzo hayo ya siku nne ambapo wengie 179 waliofika
kwa kuchelewa imeelezwa na mbunge Profesa Tibaijuka kwamba watapewa
awamu nyingine baada ya kikao cha bajeti kukamilika mwezi june mwaka huu
mkoani Dodoma
Mkurugenzi wa Lake zone Driving School mkoani Kagera Winstoni Kabantega akiongea jambo.
Kupitia Bukobawadau waendesha pikipiki hao wametoa shukrani za dhati kwa Mbunge wao Mama Anna Tibaijuka kwa kudhamini mafunzo hayo.