Bukobawadau

TAMISEMI KUWACHUKULIA HATUA WAKUU WA SHULE ZILIZOFUNGWA KWA UKOSEFU WA CHAKULA

Wakati ukosefu wa chakula ukizikumba shule za sekondari nchini za bweni na kusababisha baadhi kufungwa, Katibu mkuu TAMISEMI Dr. Jumanne Sagini amewaagiza wakuu wa wilaya kuwachukulia hatua za kisheria wakuu wa shule za sekondari za serikali zilizofungwa kwa sababu ya ukosefu wa chakula. Katibu huyo amesisitiza kwamba wakuu wa shule hawana mamlaka ya kufunga shule isipokua TAMISEMI na uongozi wa wilaya [Vyanzo: Daily News, 14/4/2015 ukurasa wa 1 na The Gurdian, 14/4/2015, ukurasa wa 1].
Bukobawadau tunaendelea kuwasiliana na Wadau wa elimu kwa lengo la kukujuza kinachoendelea mpaka sasa kutokana na Wanafunzi wa shule za sekondari za serikali za Rugambwa, Kahororo, Ihungo, Nyakato, Rukore, Kabanga na Muyenze mkoani Kagera Kurudishwa nyumbani kutokana na ukosefu wa chakula. Wanafunzi wanaojiandaa na mitihani ya taifa tu ndio waliobaki shuleni. [Chanzo: Citizen, 13/4/2015, ukurasa wa 9]. Pia imeripotiwa kuwa shule za sekondari za serikali katika mikoa ya Dodoma, Tabora, Mtwara, Arusha, Mwanza na Mbeya zinakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula [Chanzo:Tanzania Daima, 13/4/2015, ukurasa wa 2].
Nini maoni yako kuhusu maamuzi ya Katibu wa TAMISEMI ?
Next Post Previous Post
Bukobawadau