VATICAN YAMKATAA BALOZI WA UFARANSA
Mzozo wa kidiplomasia umezuka kati ya makao makuu ya papa mtakatifu ya the Vatican na Ufaransa kuhusiana na uteuzi wa balozi mpya wa Ufaransa, mjini Rome.Rais wa Ufaransa Francois Holland, amempendekeza muumini mmoja wa kanisa hilo ambaye ni mpenzi wa jinsia moja kuwa balozi wake mjini Vatican.
Lakini utawala wa Vatican umesema uteuzi huo haukubaliki.Makao makuu ya papa mjini The Vatican hayajasema lolote kuhusiana na uteuzi huo ,lakini ni dhahiri kuwa baadhi ya maafisa wakuu katika kanisa hilo hawajakubali msimamo wa papa kuhusiana na waumini wa kanisa hilo ambao ni wapenzi wa jinsia moja.
Papa alinukuliwa akihoji kuwa yeye hawezi kumhukumu mtu yeyote kwa misingi yoyote.
Serikali ya Ufaransa ilimteua laurent Stefanini kuwa balozi wake mjini vatican mnamo mwezi Januari mwaka huu.
Balozi Stefanini mwenye umri wa miaka 55,amekiri hadharani kuwa yeye anashabikia mapenzi ya jinsia moja na amewahi kufanya kazi katika ubalozi huo mjini Roma na amekuwa mshauri wa masuala ya kidini katika wizara ya mambo ya nje ya ufaransa.
Kwa sasa hakuna upande unaoonekana kuwa tayari kubadili msimamo wake.
Ufaransa ilhalalisha ndoa za jinsia moja mwaka 2013 na uamuzi wa The vatican wa kukataa kumkubali balozi Stefanini huenda ikawa ni thibitisho la The vatican la kutoidhinisha msimamo huo wa Ufaransa. VIA BBC.