WATU 6 WAMEUAWA KUFUATIA SHAMBULIZI LA CHUO KIKUU NCHINI KENYA
Mpaka sasa Watu 6 wamedaiwa kuuawa kufuatia shambulizi la chuo kikuu nchini Kenya huku wanne wakijeruhiwa
Wapiganaji waliofunika nyuso zao wameshambulia eneo la chuo kikuu cha Garissa kaskazini mwa Kenya karibu na mpaka wa taifa hilo na Somalia.Milio mikali ya risasi pamoja na milipuko imesikika katika chuo kikuu cha Garissa mjini humo.
Maafisa wa usalama wa Kenya wamethibitisha kuwa watu wawili wamefariki huku wanne wakijeruhiwa.
Wakaazi wa eneo hilo wametakiwa kukaa mbali na eneo la chuo hicho.
Haijulikani
ni nani aliyehusika na shambulizi hilo ,lakini kundi la wapiganaji wa
Somalia Al shabaab limetekeleza misururu ya mashambulizi mjini Garissa
pamoja na maeneo mengine ya Kenya tangu mwaka 2011 wakati wanajeshi wa
kenya walipopelekwa Somalia.
Hizi ni picha za matukio ya shambulizi la chuo kikuu cha mji wa Garrissa
nchni Kenya ambapo takriban watu 6 wamedaiwa kuuawa kufikia sasa.
Chanzo:BBC