KIGOMA WAPONGEZWA KWA UBUNIFU WA KUSAFIRISHA WAOMBA HIFADHI YA UKIMBIZI KUTOKA BURUNDI WANAOINGIA NCHINI
Mkuu wa mkoa wa Kigoma Kanali
Mstaafu Issa Machibya (mwenye koti) akipata maelezo ya njia ya kutembea kwa
miguu kutoka Kagunga hadi Mkigo kutoka kwa mkazi wa kijiji hicho, Mahmud Ahmad wakati
alipokagua njia hiyo ili itumike kuwasafirisha waomba hifadhi ya ukimbizi wa
Burundi, tarehe 17 Mei, 2015, (mwenye Kaunda suti ) ni Mkurugenzi Idara ya
uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig.Jen, Mbazi Msuya
Mkuu wa mkoa wa Kigoma Kanali
Mstaafu Issa Machibya (mwenye koti) akiwa katika kijiji cha Kilemba kwa ajili
ya kuwapokea waomba hifadhi ya ukimbizi
wa Burundi waliokuwa wanasafirishwa kwa kutembea kwa miguu kutoka kijiji cha
kagunga hadi kijijini hapo ili wapelekwe
kambini (mwenye Kaunda suti ) ni Mkurugenzi Idara ya uratibu maafa Ofisi ya Waziri
Mkuu Brig.Jen, Mbazi Msuya, Mkuu wa Kikosi
cha Jeshi la Wananchi 24 KJ
Kigoma, Luteni Kanali Donald Msengi (katikati) na Kaimu Katibu tawala wa
mkoa wa Kigoma, Salvatory Shauri tarehe 17 Mei, 2015.
Mkuu wa mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya akiongea na vijana ambao ni waomba hifadhi ya ukimbizi kutoka Burundi mara baada ya kuwapokea vijana hao walipofika kijijini Kilemba ili wapelekwe kambini baada ya kusafirishwa kwa kutembea kwa miguu kutoka kijiji cha kagunga tarehe 17 Mei, 2015.
Baadhi ya vijana takribani 36 ambao ni waomba hifadhi ya ukimbizi kutoka Burundi wakiwa wamepunzika kijiini Kilemba kabla ya kusafirishwa na basi kwenda kwenye kambini mara baada ya kusafirishwa kwa kutembea kwa miguu kutoka kijiji cha kagunga tarehe 17 Mei, 2015.
Mkurugenzi Idara ya uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig.Jen, Mbazi Msuya akiongea na mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la kusafirisha wakimbizi, Son Ha Dinh, mara baada ya kuwasafirisha vijana takribani 36 ambao ni waomba hifadhi ya ukimbizi kutoka Burundi kutoka kijiji cha kagunga, tarehe 17 Mei, 2015.
Mkuu wa mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya akiongea na vijana ambao ni waomba hifadhi ya ukimbizi kutoka Burundi mara baada ya kuwapokea vijana hao walipofika kijijini Kilemba ili wapelekwe kambini baada ya kusafirishwa kwa kutembea kwa miguu kutoka kijiji cha kagunga tarehe 17 Mei, 2015.
Baadhi ya vijana takribani 36 ambao ni waomba hifadhi ya ukimbizi kutoka Burundi wakiwa wamepunzika kijiini Kilemba kabla ya kusafirishwa na basi kwenda kwenye kambini mara baada ya kusafirishwa kwa kutembea kwa miguu kutoka kijiji cha kagunga tarehe 17 Mei, 2015.
Mkurugenzi Idara ya uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig.Jen, Mbazi Msuya akiongea na mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la kusafirisha wakimbizi, Son Ha Dinh, mara baada ya kuwasafirisha vijana takribani 36 ambao ni waomba hifadhi ya ukimbizi kutoka Burundi kutoka kijiji cha kagunga, tarehe 17 Mei, 2015.
Na.
Mwandishi Maalum.
Idara ya Uratibu wa Maafa
Ofisi ya Waziri Mkuu imeupongeza mkoa wa Kigoma kwa kushirikiana na mashirika
ya kimataifa yanayowahudumia wakimbizi kwa ubunifu wanaoufanya wa kusafirisha
waomba hifadhi ya ukimbizi kutoka Burundi. Kutokana na zoezi linaloendelea
mjini Kigoma la upokeaji waomba hifadhi hao, tayari waomba hifadhi wapatao elfu
90 wameandikishwa kuingia nchini kupitia kijiji jirani na Burundi cha Kagunga.
Hadi tarehe 15, Mei tayari waomba hifadhi wapatao elfu 21 walikuwa wamesafirishwa
kwa meli hadi Kigoma mjini na baadae kusafirishwa kwa basi hadi katika kambi ya Nyarugusu
wilayani Kasulu.
Kutoka kijijini Kagunga hadi Kigoma mjini usafiri unaoaminika ni
usafiri wa majini. Meli ya Mv. Liemba ambayo hutumika kubeba abiria inaouwezo
wa kubeba abiria wapatao 600. Mkoa wa Kigoma kwa kushirikiana na mashirika ya
Kimataifa wameweza kutumia meli ya kukodi ya Mv. Malagarasi kwa ajili ya kubeba
abiria yenye uwezo wa kubeba abiria wapatao 300. Aidha, kwa kuzingatia idadi kuwa
kubwa ya waomba hifadhi dhidi ya vyombo
vya usafri salama vya majini vinavyotumika, tayari njia nyingine imebuniwa ya
kutumia njia ya kutembea umbali wa km 10 kwa vijana wenye nguvu , kutoka kagunga
hadi Kilemba ambapo husafirishwa na mabasi
hadi katika kambi ya Nyarugusu wilayani Kasulu.
Mkurugenzi Idara ya Uratibu
wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Jenerali Mbazi Msuya akiongea hivi karibuni mara baada
ya kuwatembelea waomba hifadhi hao waliopo kijijini Kagunga na kushiriki zoezi
la kuwapokea waomba hifadhi hao mjini
Kigoma wapatao 600 waliowasili kwa meli
ya Mv. Liemba na kuwapokea wengine kijijini Kilemba wapatao vijana 36
waliosafirishwa kwa kutembea kwa miguu kutoka Kagunga, alisema kuwa kutokana na
idadi ya watu waliopo kijijini hapo na vyombo salama vya usafiri wa majini
vilivyomo mkoani humo ubunifu wa namna ya kuwasafirisha waomba hifadhi hao hadi
kambini ni vyema ukapongezwa.
“Takwimu za uhamiaji za
Kagunga zinaonesha kuwa hadi hivi sasa wapatao watu elfu 90 wamejiandikisha
kuingia nchini kupitia mpaka uliopo hapa
kagunga na kati ya watu hao watoto ni wapatao elfu 75 , ile hali kwa
mujibu wa mtendaji wa kijiji hiki kuna wakazi wapatao elfu 17, kwa mantiki hii
idadi hii ya watu ni kubwa ukilinganisha na uwezo wa kijiji hivyo ubunifu wa
kutumia njia ya kusafirisha vijana wenye nguvu kutembea mwendo wa km 10, hadi
Kilemba utapunguza idadi ya watu waliopo hapa na hatimaye tutakuwa nauwezekano
mkubwa wa kuepuka magonjwa ya mlipuko kijijini hapo” alisema Msuya
Aliongeza kuwa palipo na
watu wengi yakilipuka magonjwa ya
mlipuko ni maafa makubwa. Hivyo idara ya uratibu wa maafa nchini inaupongeza
uongozi wa mkoa wa Kigoma unavyofanya
zoezi hilo kwa kushirikiana na serikali ya kijiji cha kagunga , halmashauri za
wilaya pamoja na mashirika ya kimataifa yanayowahudumia
wakimbizi na Taasisi za kitaifa zinazowahudumia wakimbizi kwa kuwapokea waomba
hifadhi hawa kwa kuhakikisha wanakuwa salama.
Vilevile alifafanua kuwa
lengo ni kuepusha maafa kwa waomba hifadhi na jamii ya kitanzania hivyo tayari
wameshajadiliana na uongozi wa mkoa juu ya njia nyingine mbadala za kuharakisha
usafiriishaji wa waomba hifadhi hao ambapo kwa kuwa njia hizo zinashirikisha
wadau tofauti wenye mamlaka mbalimbali
baada ya kuwafikishia mawazo hayo njia hizo zitaanza kutekelezwa mara
moja ili kuepusha maafa yanayo weza kutokana na idadi kubwa ya watu waliopo
Kagunga.
Awali, akiongea mara baada
ya kuwapokea vijana wapatao 36 ambao ni waomba hifadhi ya ukimbizi waliotembea kwa miguu umbali wa km 10
kutoka kijijini Kagunga hadi kijijini
Kilemba Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu, Issa Machibya aliwataka waomba hifadhi ya ukimbizi kutoka
Burundi hao kutii na kufuata sheria na kanuni wanazo elezwa na uongozi husika
pindi wanapokuwa katika kambi watakazo hifadhiwa hapa nchini.
Mwisho.