KUHUSU WAKIMBIZI WILAYANI NGARA
KAMATI ya Ulinzi na Usalama mkoani Kagera leo
imefanya ukaguzi wa mpaka wake wilayani Ngara na nchi jirani ya Burundi ili
kujiridhisha na taarifa za kuingia kwa wakimbizi kutoka nchini humo wanaodaiwa
kukimbia maandamano ya kisiasa
Mkuu wa mkoa wa Kagera Bw John Mongella ambaye ni
Mwenyekiti wa kamati hiyo mkoani humo amesema
wakimbizi walioingia nchini kupitia wilayani Ngara ni raia tisa wa
Burundi walioko kijiji cha Kasange mpakani na nchi jirani ya Burundi
Mongela amesema kuwa serikali ya Tanzania kupitia
waziri wa mbambo ya ndani ndiyo yenye mamlaka ya kutangaza kuepo kwa wakimbizi
kutoka nchini Burundi na kuanza kuwapokea kisha kuwapatia hifadhi kwa ajili
ya usalama wao
Amesema
walikokutwa wakimbizi hao tisa wako mpakani na nchi yao ya Burundi
lakini wananchi wenzao wa nchi hiyo bado wanaendele na shughuli mbalimbali za
uzalishaji mali jambo ambalo halijatoa fursa kuwapokea mkoani Kagera.
“Sisi tunawaombea wenzetu wa Burundi kuishi kwa
amani na endapo wataingia tutawapokea kwa kuwa ni utamaduni wetu watanzania
kusaidia walio namatatizo ya kisiasa na changamoto nyingine za
kimataifa”Alisema Mongela
Wajumbe wa kamati hiyo ya ulinzi na Usalama wamelikagua eneo la
Lumasi wilayani Ngara kwa ajili ya
maandalizi ya awali ya kuwapokea wakimbizi ambapo liliwahi kutumika wakati wa
wakimbizi wa Burundi kati ya mwaka 1995
Katika kundi pichani ni sehemu ya Wakimbizi 9 kutoka Burundi walioko kijiji cha Kasange mpakani na nchi jirani ya Burundi.
Katika hatua nyingine Mongela ameagiza Halmashauri
ya wilaya ya Ngara kuacha mara moja kuuza maeneo na rasilimali mbalimbali
katika halmashauri hiyo ambazo zinaweza kusaidia wananchi panapotokea majanga
ya kijamii
Amesema
rasilimali hizo ni msaada wa baadaye panapotokea matatizo kama majanga
ya kuhitaji kupatikana miundombinu na kwamba eneo la Lumasi iliyokuwa kambi ya
wakimbizi 1995 hadi 2000 yameuzwa na kugawiwa wananchi
Wakimbizi tisa waliokuwa mpakani mwa kijiji cha
Kasange wilayani Ngara na nchi jirani
na Burundi wamesema waliingia Tanzania siku tatu zilizopita na kupewa hifadhi
katika kijiji hicho wakitokea mpakani na nchi jirani ya Rwanda
Wamesema wanakimbia nchi yao baada ya kuhojiwa usiku
nina kuorodheshwa majina kulazimishwa kutamka kuwa wafuasi wa chama cha CNDD
FDD na baada ya muda wanapoamka hukuta majirani zao wameondoka hivyo kujawa na
woga
Juzi mkuu wa wilaya ya Ngara Costantine Kanyasu aliliambia
gazeti hili kuwa wakimbizi 85 walioingia wilayani humo wakitokea nchini Rwanda
raia wa Burundi wamerudishwa makwao kupitia mpaka wa Kobero nchini humo
Mkuu wa idara ya uhamiaji mkoani Kagera George Kombe amesema idara hiyo inapokea na
kuwarudisha wahamiaji haramu wanaoingia
nchini kinyume na taratibu mbapo hadi Aprili 30 mwaka huu
wamerudishwa makwao wahamiaji 175
Amewahimiza
wananchi na viongozi wa vijiji wilayani Ngara kushirikiana na vyombo vya dola
kuwabaini wahamiaji haramu na kutoa taarifa sahihi endapo watakuwepo wakimbizi
kwa ajili ya kupatiwa usalama katika maeneo husika
Mkuu wa Mkoa wa Kagera akikagua maeneo yaliopo mpakani Wilayani Ngara.
NGARA:Na Shaaban Ndyamukama