MAAFA YA MVUA DAR MAY 7,2015
Mkurugenzi
mkuu wa mamlaka ya hali ya hewa nchini Dr. Agnes Kijazi amewataka
wakazi wa mikoa ya pwani kuendelea kuchukua tahadhari kufuatilia taarifa
za utabiri wa hali ya hewa kutokana na mvua hizi za msimu kuendelea
hadi mwisho wa mwezi mei ingawa mvua kubwa zinaonesha zitaendelea hadi
tarehe 20. Mikoa hiyo ni Dar es Salaam Mtwara,
Lindi,Tanga,Pwani,Unguja na Pemba.
Serikali imefunga Barabara ya Morogoro Road eneo la Jangwani Dar es salaam kufuatia Daraja kuzibwa na Maji huku barabara nazo zikifunikwa na maji.
Tandale jijini Dar es salaam (Picha imetumwa na Jeniffer)
SEHEMU YA VIDEO KUTOKA KUTOKA CHANNEL 10 MCHANA MAY 7,2015

Zaidi wa wananchi 6000 wa kata ya wazo jimbo la kawe na kata ya goba jimbo la ubungo jijini dar es salaam hawana mawasilaiano ya barabara na huduma ya UMEME baada ya mto Tegeta kufurika maji na kusomba daraja lao la muda walilokuwa wanategemea kuvukia na kusababisha shughuli za kata hizo kusimama.
Wakazi hao wamethirika zaidi kutokana na mto huo kufurika maji huku ukiendelea kulika ukizifuata nyumba za wananchi na wakazi wa mtaa wa muungano waliopo kata ya goba na mtaa wa kilimahewa waliopo kata wazo ambapo ITV imeshuhudia wakazi hao wakilazimika kuhatarisha maisha yao kwa kutumia kamba kwa ajili ya kuvuka huku nguzo ya umeme mkubwa ikiwa inaninyinia katikati ya mto huo Jambo lilolazimu shirika la ugavi wa umeme nchini kakata huduma ya umeme katika kata hizo.
Wakizungumza na ITV wakiwa wamefatana na mwenyekiti wao wa mtaa wa muungano wananchi hao wamewalaumu vingozi wao wakiwemo wabunge na viongozi wa wilaya ya kinondoni kwa kutowawekea daraja la kudumu katika mto huo na kuwasababishia adha kila mara mvua kubwa inaponyesha ikwemo ya mwaka jana.
Wakazi wengine waliokubwa na mafuriko ni wanaoishi kandokando ya mto mbezi ambapo nyumba zao zimesombwa na maji huku kingo za mto huo zikiendelea kulika na kufuata nyumba zao ambapo wameiomba serikali kuwapatia viwanja vya bei raisi sehemu nyingine.
Katika tukio lingine mvua zinazoendelea kunyesha zimesababisha visima vya mafuta kujaa maji na kusababisha baadhi ya madereva wa vyombo vya moto kukumbwa na adha kubwa ya magari yao kuzima baada ya kuwekewa mafuta yalichanganyika na maji ya mvua katika kituo cha mafuta cha kobil kilichopo afikana huku meneja wa kituo hicho akisuasua kuwalipa madereva hao.