NAIBU WAZIRI CHARLES MWIJAGE AIUNGA MKONO TIMU YA RAS KAGERA FOOTBALL CLUB KWA KUICHANGIA MILIONI MOJA ILI ISHIRIKI LIGI DARAJA LA PILI NGAZI YA KANDA
Katika kutengeneza ajira kwa
vijana na kuuendeleza mkoa wa Kagera kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo
kutoka sehemu mbalimbali na ndani ya mkoa Katibu Tawala wa Mkoa Bw. Nassor
Mnabila aliamua kuanzisha timu ya mpira
ya mkoa wa Kagera .
Madhumuni ya kuanzisha timu hiyo ni
kuuleta mkoa wa Kagera pamoja, kutoa ajira kwa vijana wenye vipaji vya michezo
aidha kuutangaza mkoa nje na ndani ya nchi kuhusu fursa za uwekezaji
zinazopatikana ndani ya mkoa wetu wa Kagera.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera
Bw. Nassor Mnambila mara baada ya
kuanzisha timu hiyo ambayo kwa sasa inajulikana kama RAS Kagera Football Club na
kuiwezesha kushiriki ligi daraja la nne na daraja la tatu na kufuzu kushiriki ligi
daraja la pili ngazi ya Kanda katika kituo cha Mbulu mkoani Manyara .
Kwa kushirikisha wadau mbalimbali
wa mkoa wa Mkoa wa Kagera hasa wapenda michezo na maendeleo ya mkoa wa wameweza
kuichangia timu hiyo ili kushiriki ligi daraja la pili ngazi ya Kanda na kama
ikifuzu itaweza kushiriki ligi daraja la pili ngazi ya taifa.
Ushiriki wa timu hiyo unahitaji
michango ya wadau kwani ni timu ya mkoa inayouwakilisha mkoa wa Kagera wadau
walioweza kuichangia timu hiyo ni pamoja na Wadau wa maendeleo toka Dar es
Salaam pamoja na Wadau wa maendeleo waliopo mkoani hapa.
Aidha wanasiasa hawakubaki nyuma
ambapo Mbunge wa Bukoba Vijiji Mhe. Jasson Rweikiza naye ameichangia kiasi cha
shilingi 300,000/- na Mbunge wa Meleba Kaskazini Naibu Waziri wa Nishati na
Madini Mhe. Charles Mwijage leo tarehe 20/05/2015 ameichangia timu hiyo
shilingi 1,000,000/-
Wadau wote wa maendeleo wa mkoa
wa Kagera mnaombwa kumuunga mkono Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera ili
kufanikisha adhima yake ya kuuendeleza mkoa huu hasa katika sekta ya michezo.
Aidha kwa wote wenye nia na mapenzi mema ya kuichangia timu hiyo wananweza
kuonana na Mwenyekiti wa kamati ya muda Bw. Seif Hssein Katibu Tawala Msaidizi upande wa Miundombinu
Ofisi ya Mkuu wa mkoa Kagera.