NGARA:MAADHIMISHO YA SIKU YA WAUGUZI
Wauguzi wilayani Ngara mkoani Kagera wametakiwa
kutumia kauli zenye kuwafariji wagonjwa
wakiwa kwenye vituo vya kutolea huduma hatimaye waweze kuaminiwa na
jamii na kuwapa matumaini ya kuishi wagonjwa wao
Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Nyamiaga wilayani
Ngara Dr Nelson Rufano ametoa wito huo
leo wakati wa maadhimisho ya siku ya wauguzi yaliyofanyika kwa kumuenzi Muuguzi
mkuu Florence Naitingaly raia wa nchini Italia
Dr Rufano amesema kuwa wauguzi ndio wanaokaa na wagonjwa muda mrefu na
kubaini changamoto zinazowakabili hivyo wakitumia lugha ya upole inaweza
kuwatia matumaini wagonjwa na waangalizi wao
Aidha Mwakilishi wa Muuguzi mkuu wa wilayani Ngara
Bi Doroth Ntakamulenga amewahimiza wauguzi hao tawi la Nyamiaga kufanya
kazi bila ya kuomba rushwa kutoka kwa
wagonjwa na kuweza kuaminika ndani ya
jamii
Kwa upande wao wauguzi wamesema wanafanya kazi
katika mazingira magumu lakini wanahita uvumilivu na subira ikiwa ni pamoja na
kufanya vikao vya pamoja kuwakemea wanaojitokeza kudhalilisha taaluma yao
Maadhimisho hayo yaliambatana na Burudani ya muziki
kwa wauguzi hao huku baadhi yao wakipatiwa zawadi ya utendaji kazi bora ambapo
Mwakilishi wa Mganga mkuu wa Wilaya ya Ngara Bw Patrick Ogo amewataka wauguzi kujituma na kuepuka kufanya kazi kwa mazoea bali
wajiendeleze kitaaluma
Maadhimishoya siku ya wauguzi hufanyika kwa kujumuisha wauguzi wa
zahanati .vituo vya Afya na Hospitali za serikali na taasisis binafsi
lakin kwa mwaka huu wilayani Ngara yameadhimishwa kwa kila taasisi
kutokana na ukata wa kifedha na wahusika zaidi kuhudhuria maadhimisho
hayo kwa ngazi ya Kitaifa.
Katika picha matukio ya Burudani yakiendelea.