WAHITMU WA MAFUNZO YA SHERIA ZA USALAMA BABARANI WAMSHUKURU MAMA TIBAIJUKA
Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini Prof. Tibaijuka akiongea na Waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda walio hitimu mafunzo ya sheria za usalama barabarani ambapo amewataka kuwa makini pindi wawapo barabarani ili kujiepusha na ajali.
Amesema wilaya ya Muleba imebainika kuwa na na madereva 60 wanaoendesha magari na pikipiki zaidi ya miaka 20 iliyopita bila kuwa na leseni na hao mara nyingi wamekuwa wakisababisha ajali kwa uzembe ulevi na mwendo kasi
WAHITIMU wa mafunzo ya sheria za usalama
barabarani kutoka jimbo
la Muleba kusini Mkoani Kagera wamelitaka jeshi la polisi kuelimisha zaidi bodaboda madhara ya kuvunja
sheria ili kuepuka kufanya kazi kwa mazoea
Wakisoma risala ya kuhitimu mafunzo hayo jana yaliyoanza
April 27 mwaka huu wamesema katika mafunzo yao waendeshaji vyombo vya moto
walikuwa 422 kati yao wanawake watatu waliojifunza
sheria na matumizi bora ya barabara,Mwenyekiti wa wahitimu hao Bwana Sildion
Bushaijabwe amesema kabla ya mafunzo ya kutambua sheria na matumizi ya alama za
usalama barabarani waendeshaji wa vyombo
vya moto walikuwa wakitengeneza mazingira ya uadui na askari polisi
Bwana Bushaijabwe amesema matukio ya ajali maeneo mengi
nchini yanasababishwa na uzembe, woga wa kukutana na askari wa jeshi la
polisi wakiwa katika shughuli za
kawaida na kwamba hali hii ilivunja mahusiano yao na bodaboda hao
Aidha
wametoa shukrani kwa mbunge wa jimbo hilo Profesa Anna Tibaijuka
kuwapatia ufadhili wa mafunzo hayo na kwamba kwa sasa wameondoa hofu ya
kukutanana askari polisi wakiwa kwenye utekelezaji wa majukumu yao
Kwa pande wake Mwenyekiti wa kamati ya usalama
barabarani mkoani Kagera Wiston Kabantega amewahakikishia
vijana hao kuwafanyia mchakato wa
kuhakikisha waendesha pikipiki wanapata
leseni na kufanya kazi kwa uhuru,Amedai kuwa pamoja na mafunzo hayo waliopata vyeti ni washiriki 408 na wengine
48 wameshindwa mitihani na kukosa sifa za kutafutiwa leseni na kwamba vijana 14
walitoroka mafunzo na kukosa fursa za
kupata vyeti na ujuzi wa sheriaAmesema wilaya ya Muleba imebainika kuwa na na madereva 60 wanaoendesha magari na pikipiki zaidi ya miaka 20 iliyopita bila kuwa na leseni na hao mara nyingi wamekuwa wakisababisha ajali kwa uzembe ulevi na mwendo kasi
Pamoja na hayo vijana hao wamesisitizwa kuhakikisha wanabeba abiria
mmoja katika pikipiki na kuwa na kofia maalum ya usalama wa vichwa vyao na abiria ili kuchukua tahadhari mara
kukitokea hitilafu ya chombo katika safari zao.
Profesa Tibaijuka amesema chanzo kikubwa cha ajali kimekuwa ni
mwendo kasi , kutozingatia sheria za usalama barabarani na kutotambua matumizi
ya alama jambo ambalo linatakiwa kufikia tamati
na kuendesha vyombo hivyo kwa usalama zaidi ndani na nje ya jimbo hilo