WORLD LUNG FOUNDATION YAZINDUA MRADI WA ELIMU KWA MTANDAO INAYOSAIDIA KUOKOA MAISHA YA AKINA MAMA NA WATOTO
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Seif
Rashid (katikati), akizungumza na waandishi wahabari mara baada ya
kuzindua mradi wa elimu kwa mtandao unaosaidia kuokoa maisha ya mama na
mtoto ambao unaendeshwa na kusimamiwa na Shirika la World Lung
Foundation (WLF) la hapa nchini, ambapo vituo vya Afya 13 vinanufaika na
mradi huo.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Seif
Rashid, akizindua mradi wa elimu kwa mtandao unaosaidia kuokoa maisha ya
mama na mtoto ambao unaendeshwa na kusimamiwa na Shirika la World Lung
Foundation (WLF) la hapa nchini, ambapo vituo vya Afya 13 vinanufaika na
mradi huo.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Seif Rashid (wapili kulia), akipiga makofi mara baada ya kuzindua mradi wa elimu kwa mtandao unaosaidia kuokoa maisha ya mama na mtoto ambao unaendeshwa na kusimamiwa na Shirika la World Lung Foundation (WLF) la hapa nchini, ambapo vituo vya Afya 13 vinanufaika na mradi huo.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Seif
Rashid (wapili kulia), akiwa na baadhi ya watendaji wa Shirika la World
Lung Foundation (WLF) la hapa nchini wakishudia uzinduzi wa mradi wa
elimu kwa mtandao unaosaidia kuokoa maisha ya mama na mtoto ambao
unaendeshwa na kusimamiwa na shirika hilo katika vituo vya Afya 13.
* Dk Seif Rashid, Waziri, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi *
(6
Mei 2015, Dar es Salaam, Tanzania na New York, Marekani) - Katika hafla
ya leo jijini Dar es Salaam, World Lung Foundation (WLF) Tanzania
ilizindua mradi wa elimu kwa njia ya mtandao katika hatua mpya ya
kusaidia kuboresha ubora wa huduma za wajawazito pamoja na akina mama na
watoto wao. Mradi huu wa Mawasiliano umefadhiliwa na Shirika la
Maendeleo la Sweden (Swedish International Development Cooperation,
(Sida)) na Shirika la Merck For Mothers. Mradi huu upo katika vituo vya
afya 13 vinavyo fadhiliwa na WLF katika mikoa ya Kigoma, Pwani na
Morogoro.
Mfumo
huu wa WLF Tanzania wa elimu kupitia mtandao (e-learning) umeundwa ili
kuboresha ujuzi wa wafanyakazi wa vituo vya afya na kuongeza wao uwezo
wa kufanya maamuzi sahihi katika kliniki zitoazo huduma za afya. Mfumo
huuutawasaidia kufanya maamuzi ya kitaalam kuhusu usimamizi wa dalili
hatarishi za ujauzito, huduma wakati wa kujifungua na baada ya
kujifungua kwa ajili ya akina mama na watoto wao.Mafunzo haya
yatawawezesha watoa huduma ya afya kuwasiliana na kupata taarifa muhimu
za kuongeza ujuzi, kusoma Makala za jarida za kitaalam, kuona filamu
zinazoelimisha, picha na masomo ya kujifunzia. Wafanyakazi wa afya pia
wanaweza kutumia jumuishi ya vikao vya mitandao na kubadilishana ujuzi
na taarifa kuhusu changamoto na mafanikio yao pamoja na wenzao na
wataalam waandamizi katika vituo vya afya 13.
“Tunaiomba
serikali kuharakisha upatikanaji wa mtandao yaani intaneti vijijini ili
tuweze kuunganisha vituo vya afya kupitia mkongo wa taifa, ili vituo
vingi vya afya viweze kutumia mradi huu kwa njia ya gharama nafuu,
"alisema Dk Nguke Mwakatundu, Mkurugenzi wa Tanzania, World Lung
Foundation. "Uwekezaji kama huu unaweza kusaidia kuokoa maisha ya mama
wengi zaidi na watoto wao."
Programu
hii ya elimu kwa njia ya mtandao ni maendelezo ya uboreshaji
unaofanywa na WLF na sehemu ya mkakati wa matumizi ya miradi wa ICT ili
kusaidia kuboresha matokeo ya afya.
Jamii ya huduma na kujifunza
Vituo
13 vya afya vilivyounganishwa na mfumo huu ni pamoja na Kituo cha Afya
cha Kibiti na Hospitali ya Wilaya Utete katika wilaya ya Rufiji, Mkoa wa
Pwani. Katika Mkoa wa Morogoro, vituo vya afya ni pamoja na Kituo cha
Afya cha Mlimba kilichopo katika wilaya ya Kilombero , na Mtimbira na
Mwaya vituo vya afya na Hospitali ya Wilaya ya Mahenge Ulanga. Katika
mkoa wa Kigoma, vituo vya afya ni pamoja na Kituo cha Afya Nguruka
katika wilaya ya Uvinza, Kituo cha Afya cha ujiji na Hospitali ya Mkoa
Maweni Kigoma mijini wilaya, Hospitali ya Wilaya ya Kasulu, Hospitali ya
Wilaya ya Kibondo na Mabamba Kituo cha Afya katika Kibondo wilaya na
Kakonko Kituo cha Afya katika wilaya ya Kakonko . Pamoja na haya, vituo
viwili vyaafya katika mkoa wa Kigoma - Kituo cha Afya cha Buhingu katika
wilaya ya Uvinza ya na Kituo cha Afya cha Nyenge katika wilaya ya
Kasulu – wataunganishwa na mpango huu mbunifu wakati marekebisho ya
kiufundi yatakapokamilika.