Dk.Shein achukua fomu ya Urais Z'bar
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akionesha mkoba wa wenye fomu kuomba ridhaa kwa Chama cha Mapinduzi
kumteuwa kuwa mgombea Urais wa Zanzibar baada ya kukabidhiwa Fomu hizo
katika Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja leo Juni 18,2015.[Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipozungumza na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi waliofika katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja leo alipofika kuchukua fomu
za kuomba ridhaa kwa Chama cha Mapinduzi kumteuwa kuwa mgombea Urais wa
Zanzibar,(kushoto)Mama Mwanamwema Shein na Makamu wa Pili wa Rais wa
zanzibar Balozi Seif Ali Iddi,(kulia)Mwenyekiti wa CCM Mkoa Kaskazini
Unguja Haji Juma na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar VuaiAli Vuai.
Viongozi wa Chama cha Mapinduzi waliofika katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja wakisherehekea wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokwenda kuchukua fomu
kuomba ridhaa kwa Chama cha Mapinduzi kumteuwa kuwa mgombea Urais wa
Zanzibar katika Ofisi ya CCM Kisiwanndui Mjini Unguja leo.