DOZI YA LEO:WEWE NI BABA JINA AU BABA MAJUKUMU???
Fatherhood is not claimed by words but action, kukubalika na kuheshimika
kama baba nyumbani kwako hakuji kwa kuwalazimisha wanao na wote waishio
ndani kwako wajue kuwa wewe ndiyo baba wa nyumba bali kwa matendo
halisi yanayotegemewa kila baba kuyafanya. Sasa unakuta mwanaume mzima
hafanyi yale ambayo baba anatakiwa kufanya, watoto au wengine hapo ndani
wakiihamishia heshima kwa mama au mtu mwingine utasikia mtu anaanza kung’aka.
Ngoja nikwambie, watoto wadogo hata kama wana umri mdogo huwa wanajua
majukumu yanayotegemewa kutoka kwa baba au mama, sasa mmoja asipofanya
majukumu yake watoto, dada wa kazi, kaka wa kazi au wengine huwa
wanajua. Ukiona mwanaume amefikia kujitambulisha kwa watoto wake kuwa
“mimi ndiyo baba wa hii nyumba, hakuna baba mwingine hapa” ujue
kashashindwa kazi huyo - Chris Mauki