Dr Harrison Mwakyembe achukua fomu za kuwania Urais kupitia CCM
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Harrison Mwakyembe ameingia leo rasmi katika kiny’ang’anyiro cha kuwania urais, kwa kuchukua fomu Mjini Dodoma kuomba ridhaa ya CCM kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa Oktoba, mwaka huu.
Dk. Mwakyembe ambaye anakuwa mwanachama wa 37 wa CCM kuchukua fomu amesema akipatiwa ridhaa ya kuwania urais atatekeleza Ilani ya CCM, na pia atapambana na rushwa kwa nguvu zake zote kama alivyokuwa anafanya akiwa katika nyadhifa zote alizoshika serikalini.