Bukobawadau

HARAMBEE YA UCHANGIAJI MAABARA SEKONDARI YA KASHENYE YAFANA

Diwani wa Kata Kashenye(Omulangira)Adeodatus Rugaibula akitoa taarifa ya maendeleo ya kata yake siku ya harambee.
 Mmoja wa watia nia ya kugombea Jimbo la Nkenge Ndugu Florent Kyombo akitoa neno.
 Pichani katikati mwenye miwani ni Balozi Diodorus,Mwenye nia ya kugombea ubunge wa jimbo la Nkenge.
 Mr Divo Rugaibula pichani kushoto
Taswira mbalimbali eneo la tukio
Sehemu ya Waalikwa wakijongea kuchangia
 Mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya Missenyi,Elizabeth Kitundu,akitoa neno
 Mdau Stephe Kyaruzi wa World map Consultant ya Dar(kushoto) na kulia ni M.C wa siku hiyo ya harambee,Lucius Kikaka wa Kikaka
ZAIDI y ash milioni 11.5 zimechangwa na wadau mbalimbali wa maendeleo wakiwemo wananchi wa Kata ya Kashenye,wazawa wa kata hiyo waishio ndani na nje ya Mkoa wa Kagera,na baadhi ya wale wanaoonesha nia ya kuwania ubunge wa Jimbo la Nkenge kupitia CCM ,katika kuchangia ujenzi wa maabara ya shule ya sekondari Kashenye,katika HARAMBEE iliyoandaliwa tarehe  13 Juni na diwani wa Kata hiyo,mh.(Omulangira)Adeodatus Rugaibula katika viwanja vya shule ya msingi Bukwali.
Miongoni mwa wachangiaji wakubwa wamekuwa BaloziDiodorus Kamala,Florent Kyombo na Julius Rugemalira(aliwakilishwa),huku diwani wa kata hiyo akisema muda ukifika atatangaza nia ya kuwania tena udiwani wa kata hiyo kupitia CCM.
Kiasi cha  milioni 84 ndizo zilikuwa zikihitajika ilI kukamilisha mahitaji  ya sh zaidi ya milioni 120 ikiwa ni ujenzi na vifaa vya maabara hiyo ya Kashenye sekondari,na wadau wameahidi kufanya jitihada kuhakikisha maabara inakamilika kwa wakati ambapo mwisho wa kukamilisha maabara zote nchini,kwa mujibu wa tamko la Rais Jakaya Kikwete ni 30 Juni mwaka huu.
NA MUTAYOBA ARBOGAST,BUKOBAWADAU-Missenyi
Next Post Previous Post
Bukobawadau