Jeshi la Polisi Iringa lakamata DVD zenye mafunzo ya Al Shaabab zikitumika na watoto wa mitaani.
Jeshi la Polisi mkoani Iringa limekamata mikanda ya DVD yenye mafunzo
ya kijeshi yanayohusiana na kikundi cha ugaidi cha Al Shaabab cha
nchini Somalia zilizokuwa zikitumika na watoto wa mitaani wanaodaiwa
kuwa walikuwa wakichukua mafunzo kwakutumia DVD hizo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa ACP.Ramadhan Mungi ametoa taarifa
hiyo mbele ya waandishi wa habari akieleza kuwa mikanda hiyo ilikuwa
ikitumiwa na vijana hao wanne wenye umri kati ya miaka 12 na 16
inaonesha ukatili na mauaji yanayodaiwa kufanywa na kikundi cha kigaidi
cha Al Shaabab mikanda ambayo walikuwa wakiitazama kwa kutumia kompyuta
mpakato yaani laptop.
Aidha kamada Mungi amesema pamoja na mikanda hiyo ya DVD pia jeshi
hilo limekamata watu wawili wanaojihusisha na biashara ya bangi wakiwa
na magunia matatu ya bangi katika harakati za kufunga bangi hiyo kwenye
vifurushi vidogo tayari kuisambaza kwa wateja wao.
Mungi ameongeza kamata hiyo iliyofanywa na jeshi hilo mkoa wa
Iringa pia imekamata nguzo 35 za umeme za shirika la umeme nchini
Tanesco nyaya za kusambaza umeme na vifaa vingine zikiwa zimehifadhiwa
kwa watu binafsi wawili ambao hakuwataja majina kwa sababu za
kiupelelezi.
ITV