Lembeli aitabiria CCM anguko katika uchaguzi mkuu utakao fanyika Octoba mwaka huu.
Mbunge wa Kahama James Lembeli
amesema viongozi wa CCM wasipo badili tabia ya kutembea na viongozi
mifukoni na kugawa kadi feki kwa watu wasiyo wanachama wa CCM kwa lengo
la kutaka kuwaengua wagombea wanao kubalika na kuweka wao CCM itegemee
kupoteza majimbo na kata nyingi katika uchaguzi mkuu ujao kwakuwa
watanzania wa leo hawadanganyiki na wajue kuwa kura inapigwa na watu
wengi siyo wana CCM pekee.
Mhe. Jamse Lembeli ametoa kauli katika mkutano wa hadhara wilayani
kahama kufuatia malamiko ya wananchi waliwakilisha katika mkutano na
kudai kuwa kumekuwepo na baadhi ya viongizi wa CCM wanapita na wagombea
na kuwalazimisha wananchi wawapigie kura na kugawa kadi feki kwa watu
wasiyo wanachama ili kuwang’oa viongozi wapinga ufisadi.
Ndipo ukifika wakati kwa Mhe. James Lembeli kusema wilaya ya kahama
imetapakaa kadi feki za CCM na kutoa angalizo kwa viongozi wa CCM kuwa
wasipo badilika watavuna mabuwa kwani watanzania wa sasa siyo wa wakati
uliyopita hivyo CCM inapaswa kuwa makini kwani hata hivyo viongozi hawo
wamekiuka tamko la makamu mwenyekiti wa CCM taifa mzee PHILIPO MANGULA
alilolitoa mkoani dodoma.
Katika mkutano huo pia wananchi walipata nafasi ya kueleza kero zao
zikiwemo za watendaji kulazimisha wawekezaji kuweka katika maeneo
ambayo wananchi hawakuridhia kuyatoa na baadhi ya wanawake kulalamikia
huduma mbovu za afya na rushwa kwa wajawazito na watoto katika
hospitali na vituo vya afya.
ITV