Bukobawadau

VIDEO/PICHA MAZISHI YA 'OMLANGIRA' SIMON BENEDICTOR KYARUZI -JUNE 12,2015 BUHEMBE -BUKOBA

 Muonekano wa picha ya Marehemu Omlangira Simon Benedictor Kyaruzi enzi za uhai wake
Marehemu ameacha Mjana Mama Regina Kyaruzi na watoto watano ambao ni James Kyaruzi, Edgar Kyaruzi, Edimund Kyaruzi, Magreth Kyaruzi na Rogders Kyaruzi aliyepo nchini Marekani, Timu nzima ya Bukobawadau Blog tunawapa pole wafiwa wote ,Mwenyezi Mungu awajaalie subira na sote atupe khatma njema
 Jeneza lenye mwili wa Marehemu Omlangira Simon Benedictor Kyaruzi likiingizwa kaburini .
 Hii ndiyo safari ya Mwisho ya Maisha ya Mlangira Simon Benedictor Kyaruzi
 Mjane wa Marehemu Omlangira Simon Benedictor Kyaruzi akiweka udongo kaburini.
 Mzee Mpanju mara baada ya kuweka Udongo kaburini.
 Mzee Baruti akiweka Udongo kwenye kaburi la Marehemu rafiki yake, Mlangora Simon.
 Marehemu Omlangira Simon Benedictor Kyaruzi alizaliwa tarehe 1.1.1945 katika Kijiji cha Binsi na kupata ubatizo tarehe 8.4.1946 katika kanisa la Kashozi na aliweza kupata kipaimara mnamo mwaka 1953.
Jeneza lenye mwili wa Marehemu Mlangira Simmon Benedictor Kyaruzi likiwa Kaburini.
 Shughuli ya mazishi yaliyofanyika jioni ya leo June 12,2015 Nyumbani kwa marehemu  Kijijini Kyaruyomba - Buhembe kilometa chache nje ya Mji wa Bukoba.

 Utaratibu wa kuweka Udongo kwenye Kaburi ukiendelea.
 Hakika ni Majonzi makubwa kifo cha Mlangira Simon Benedictor Kyaruzi aliyetutoka tarehe  9.6.2015 baada ya kuugua kwa kipindi kifupi.
Wadau mbalibali wakishiriki maziko haya kikamilifu
 Poleni sana wafiwa,tunamuomba Mwenyezi Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu mpendwa wetu.
 Padri akiinua juu Msalaba.
 Padre akiweka msalaba kwenye kaburi la marehemu Omlangira Simon Benedictor Kyaruzi
 Zoezi la kuweka mashada katika Kaburi likiendelea.
 Ma Regina Kyaruzi ambaye ni Mjane wa Marehemu akiweka shada la maua
 Fr.Isdory na Fr. Kyaruzi wakiongozi shughuli ya mazishi hayo, yalofanyika Nyumbani kwa Marehemu Kijijini Kyaruyomba - Buhembe kilometa chache nje ya Mji wa Bukoba na kuhudhuriwa na watu wengi kutoka maeneo mbalimba.
 Mr.& Mrs Edgar Simon Kyaruzi wakiweka shada la maua.
Utaratibu wa kuweka mashada ya maua ukiendelea.
Padri akiendelea kuongoza shuguli ya Mazishi
Sehemu ya waombolezaji katika hali ya majonzi
 Historia fupi ya Marehemu inasomwa na mwanae Mkubwa Ndugu Edmund Kyaruzi kama utavyo pata kumsikia na kuona katika sehemu ya Video hivi punde.
 Ndugu Edgar Kyaruzi mtoto wa Marehemu Omlangira Simon Benedictor Kyaruzi akitoa neno la shukrani kwa niaba ya familia. 
Tuwe wote hadi mwisho wa Ukurasa huu, upate kuona na kusikia maneno ya familia kupitia katika sehemu ya Video iliyo ambatanishwa mishoni mwa matukio ya picha.
 Rambirambi kutoka kwa wanachama wa Marehemu Mlangira Simon Benedictor Kyaruzi
 Neno la Kimila kutoka kwa Kaka Mdogo wa Mjane, Bi Regna Kyaruzi
 Muendelezo wa matukio katika sughuli ya Mazishi ya Marehemu Mlangira Simoni aliyepata elimu yake ya msingi katika shule ya Ihungo mnamo mwaka 1952 na kuendelea na Middle School katika shule ya Kiteyagwa mpaka kufikia mwaka 1959.
 Historia ya  Marehemu Mlangira Simon Benedctor Kyaruzi inaonyesha alipata elimu yake ya sekondari katika shule ya Ihungo  mwaka 1960-1964.
 Baada ya Elimu yake ya Sekondari, alijiunga na chuo cha Uhasibu Mzumbe na kutunikiwa stashahada mwaka 1968 na kuendelea na kozi zaidi nchini Uholanzi kabla ya kurejea nchini kulitumikia Taifa katika Idara mbalimbali kama shirika la mazao la Taifa na Shirika la meli za mwambao yaani (TACOSHILI) Tanzania Coastal  Shipping line mpaka alipo staafu mwaka 1993.
 Haya na mengineyo ni kupitia mtandao wetu wa Bukobawadau.
 Wanakwaya wa Kanisa la Bulugo Wanakwaya wakiimba nyimbo za maombolezo wakati wa Ibada ya Mazishi ya Marehemu Omlangira Simon Benedictor Kyaruzi
 Neno la bwana kutoka katika Bibilia.
 Ibada ikiendelea.
Simanzi kubwa Mjane wa Marehemu akitoa heshima zake za mwisho.
 Vilio na vikitawala wakati wanafamilia wakitoa heshima za mwisho kwa mpendwa wao.
 Taswira wakati wanafamilia wakitoa heshima zao za mwisho.
Bwana Edmund Kyaruzi akimuonyesha mwanae Mwili wa Marehemu Babu yake
Haya ndiyo yaliyojiri katika mazishi ya Mzee wetu Mlangira Simon Benedictor Kyaruzi
Wakristo walioamini  Katika kupata komonio
 Hakika ni Simanzi kubwa kwa wote waliomjuwa Marehemu Mlangira Simon Benedictor Kyaruzi
Sehemu ya Video inapatikana mwisho kabisa ya Ukurasa huu.
 Matukio mbalimbali yaliyojiri wakati Ibada ya maziko ikiendelea.
 Sehemu ya watu katikakushiriki Ibada maalumu ya kumuombea Marehemu.
 Katika kumfariji Mjane.

Kwa namna isiyoweza kuelezeka huzuni na majonzi vilitawala muda wote kwa wanafamilia kufuatia kuondokewa mpendwa wao Marehemu Mlangira Simon Benedictor Kyaruzi

Mmoja wa waombolezaji kama anavyo onekana pichani.
 Mwisho wafiwa wakielekea ndani mara baada ya shughuli ya mazishi haya.
 Sehemu ya waombolezaji Wakati wa huduma ya Chakula.
 Baadhi ya waombolezaji waliofika kwenye msiba huu wakipata chakula.
Harakati za hapa na pale muda mchache kabla ya Shughuli ya Ibada.
 Madre watatu wakiwa tayari kuongoza Ibada maalum ya kumuobea Marehemu Mlangira Simon Kyaruzi
Sehemu ya Wanafamilia mwanzoni kabisa mwa shughuli ya Ibada ya kumuaga Mpendwa wao
Wafiwa wakiwa na nyuso za huzini
Kumbuka kujiunga katika ukurasa wetu wa facebook kwa matukio mengi ya picha zaidi kupitia linki hii>>>Bukobawadau Media
  PITIA SEHEMU KAMILI YA VIDEO HAPA CHINI


 Bwana alitoa na bwana alitwa jina la bwana libarikiwe Ameen!!
 MATUKIO YA PICHA 200 ZAIDI YANAPATIKANA KATIKA UKURASA WETU WA FACEBOOK KWA KULIKE UKURASA HUO KUPITIA LINK HII>>BUKOBAWADAU MEDIA
Next Post Previous Post
Bukobawadau