Bukobawadau

MBOWE AJAPOTEZA SIFA YA KUGOMBEA URAIS,UBUNGE

Na Happiness Katabazi
JUNI 17 Mwaka huu, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Hai, Denis Mpelembwa alimhukumu Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kulipa faini ya Sh milioni Moja au kwenda jela mwaka mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kumshambulia mwangalizi wa Uchaguzi Mkuu mwaka 2010 na Mbowe alilipa faini hiyo.
Mbowe alikuwa anakabiliwa na mashtaka ya kumfanyia shambulio , mwangalizi wa ndani wa Uchaguzi Mkuu Mwaka 2010, Nassir Yamin katika kituo cha kupigia kura kilichokuwa katika Zahanati ya Lambo.
Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mpelembwa alisema kitendo kilichofanywa na Mbowe hakikubaliki na kinapaswa kukemewa.
Tangu hukumu hiyo itolewe ,kumezuka mjadala Katika Jamii na vyombo Vya Habari ambapo kundi Moja linadai hukumu hiyo imepotezea sifa Mbowe ya Kugombea nafasi ya Ubunge na urais endapo Atakuwa na nia ya Kugombea nafasi hiyo na kundi jingine linadai hukumu hiyo haijamuondolea sifa ya Kugombea nafasi hizo pindi akitaka Kuigombea nafasi hizo za uongo.
Binafsi kupitia makala hii naungana na wale wote wanaodai Kuwa hukumu hiyo haijamuondolea sifa ya Kugombea nafasi ya rais,Ubunge pindi akitaka Kugombea nafasi hizo.
Makala yangu hii kabla ya kwenda Mbali imetazama aina ya makosa aliyotiwa nayo hatiani Mbowe.
Pia nimefanya utafiti wangu wa kisheria kuona Je makosa hayo aliyotiwa nayo hatiani Je ni makosa yanaangukia Katika Ibara ya 39 na 67 ya Katiba ya Jamhuri Muungano ya Mwaka 1977 ? Kwani Katika Ibara hizo kuna aina ya makosa ambayo yameanishwa wazi Kuwa endapo MTu atatiwa hatiani na makosa ya aina hiyo atakuwa amepoteza sifa Kugombea urais au Ubunge.
Ibara ya 39 (e) ya Katiba hiyo inasomeka hivi ; " katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya
Uchaguzi Mkuu. hajawahi kutiwa hatiani katika Mahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyote ya Serikali;
Ibara ya 67(2) (c) Ikiwa mtu huyo amehukumiwa na Mahakama yoyote katika Jamhuri ya Muungano na kupewa adhabu ya kifo au ya kufungwa gerezani kwa muda unaozidi miezi sita kwa kukutwa na hatia ya kosa lolote, vyovyote linavyoitwa, linaloambatana na utovu wa uaminifu; au
Ibara 67(2) (d) ikiwa katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya Uchaguzi Mkuu amepata kuhukumiwa na kupewa adhabu ya kifungo kwa kosa linaloambatana na utovu wa uaminifu au kwa kuvunja sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma".
Kwa mujibu wa Ibara hizo mbili ni wazi kabisa makosa aliyotiwa nayo hatiani Mbowe hayaangukii Katika Ibara hizo mbili na kwa maana hiyo Mbowe licha ametiwa hatia kwa kosa la shambulio ,sio kosa la kukwepa kulipa kori kwa serikali,kosa la kukosa uaminifu.
Hivyo Mbowe anayohaki ya Kugombea nafasi hizo pindi akitaka kwasababu Katiba haikulitaja kosa la shambulio Kuwa endapo mtu atapatikana na kosa basi hataruhusiwa Kugombea nafasi hizo.
Pia nimejiuliza Je adhabu aliyopewa Mbowe Juzi inamzuia Kugombea nafasi ya Rais au Ubunge pindi akitaka kufanya hivyo?
Baada ya kujiuliza pia nilifanya utafiti wangu kisheria ambapo nimebaini Adhabu ile ya kulipa faini ya Sh.milioni Moja haimzui pia Kugombea nafasi hizo Kama anaitaji Kugombea .
Kwa Sababu Ibara ya 67 (7) ya Katiba inasomeka hivi; Kanuni zifuatazo zitatumika kwa ajili ya ufafanuzi wa aya ya ( c), ya (d) na ya (e) za ibara ndogo ya (2) ya ibara hii, yaani-
(a) ikiwa mtu amepewa adhabu mbili au zaidi za kufungwa gerezani na imeamuliwa afungwe kwa muda wa mfululizo, basi adhabu hizo zitahesabiwa kama ni adhabu mbalimbali iwapo muda uliotajwa katika kila moja ya adhabu hizo hauzidi miezi sita; lakini iwapo muda uliotajwa katika adhabu yoyote kati ya adhabu hizo unazidi miezi sita basi adhabu hizo zote zitahesabiwa kama ni adhabu moja; zitahesabiwa kama ni adhabu moja;
(b) ikiwa mtu atapewa adhabu ya kufungwa gerezani
ikifahamika kuwa adhabu hiyo ya kifungo imetolewa badala ya adhabu ya kutozwa faini au imetolewa kwa sababu mtu huyo ameshindwa kulipa faini aliyoamriwa kulipa, basi muda wa kifungo cha namna hiyo hautahesabiwa.
Kwa Tafsiri nyepesi Ibara ya 67(a)(b) zinazungumzia muda wa Kifungo. Na Mbowe hajatumikia Kifungo gerezani maana alilipa faini .
Na hata Kama kosa alilotiwa nalo hatiani Mbowe la shambulio lipo Katika Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, bado haiwezi kumwondolea sifa Mbowe ya Kugombea nafasi hizo Kwani Mbowe hajatumikia Adhabu ya Kifungu kwa muda usioidi Miezi Sita Kwani Mbowe alilipa faini .
Kwa Tafsiri ya Ibara hizo hapo juu nilizozitaja hapo juu Katika makala yangu hii , Mbowe sio kweli Mbowe amepoteza sifa za Kugombea urais au Ubunge.
Mbowe naamini hukumu hiyo itakuwa imekupa funzo la kuacha kujichukilia Sheria mkononi Kwani hukumu hiyo imekutia doa Kuwa wewe ni kiongozi wa kisiasa mwenye hadhi ya Ubunge, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bunge na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( Chadema), lakini ukashindwa kutii Sheria bila shuruti ukaamu kujichukulia Sheria mkononi na kuamua kumpiga Mkurugenzi wa Uchaguzi Mwaka 2010.
Kwa Mara Kadhaa nilikuwa nikiandika makala mbalimbali za kukemea baadhi ya matendo ya Uvunjifu wa Sheria yaliyokuwa yakufanywa na baadhi ya wanachama wa Chadema yakiwemo makosa ya kuandamana bila kutoa taarifa Polisi,nanilikuwa nikikemea vitendo hivyo na Kama kawaida Yao walikuwa wakinupitukana minilikuwa madharau kwasababu niliwaona ni wajinga ambao hawafahamu Sheria za nchi zipo ,zitatumika na Hazina macho zinatakiwa kukuadhibu mtu yoyote Yule anayepatikana na hatia ya kuzivunja.
Na kweli Juni 17 Mwaka huu,sote ni mashahidi Sheria hizo hizo ambazo baadhi ya wafuasi wa Chadema wamekuwa wakidai ni Sheria Mbaya mara nzuri zilimtia adabu Mbowe kwani zilimia hatiani.
Licha Sheria hizo hizo wanazodai ni Mbaya siku Mahakama ikizitumia kutoa hukumu Katika baadhi ya Kesi zinazowakabili wanachama wa Chadema na wanachama Hao wakashinda Kesi hizo wanachama hao usema Mahakama imetenda Haki ila siku Mahakama ikitumia Sheria hizo hizo kuwaita hatiani baadhi ya wafuasi wa Chadema, wafausi hao ulalamika na Kusema Mahakama ni a CCM na wamuonewa. Ajabu..
Kama Utakumbuka makala yangu ya Mwaka Jana iliyokuwa na kichwa cha Habari kisemacho " DOZEE DOZEE FREEMAN MBOWE ' ndani ya makala hiyo nilikuasa sana kuheshimu Sheria za nchi Kwani Sheria zinakutaka wewe na wananchi wote kuheshimu Sheria.
Na hukumu hiyo naamini umeamini hata kimoyo moyo Kuwa Sheria zipo, Hazina macho na zimekushughulikia.Pole sana ,ila nakushauri hukumu hiyo iwe ni Funzo kwako na usirudie tena Kutenda matendo hayo ya kihuni ya kumpiga mtu ambayo tunatazamia anayefanya makosa ya aina hiyo ni wahuni na siyo MTu mwenye hadhi ya Kama yako.
Mbowe Mzee wangu hivi sasa jitambue Kuwa umeishakuwa Mtu mzima ,mambo mengine Kama haya ya kihuni huni ya kujichukulia Sheria mkononi ,kutoa maagizo ya kwa wanachama wako wafanye maandamano bila kikomo tena bila kutoa taarifa Polisi achana nayo Kwani mwisho wa siku yanakushushia heshima wewe na familia yako na Chama unachokiongoza.
Ni wazi kabisa haipendezi Kuwa Mwanachama wa Chama Fulani halafu Mwenyekiti wa Chama hicho anashitakiwa na kukutwa na hatia ya Kutenda kosa Kama Hilo lako ulilotiwa nalo hatiani.
Ni aibu sana ,licha unaweza kujitutumua Mbele za watu Kuwa hujali ila ukweli ni kwamba hukumu hiyo imekutia doa.
Jirekebishe,kuna vitu vingine Kama hivi Vya kihuni huni acha usivifanye maana vinashusha heshima yako ndani na nje ya nchi na siyo sifa ya kila siku kiongozi Kama wewe,mfanyabiashara mkubwa Kutwa kushinda kwenye vyumba Vya Mahakama ukikabiliwa na Kesi za kipuuzi puuzi ambazo zilipaswa zifanywe na watu wasiyo na hadhi Kama yako Katika Jamii.
Ibara ya 13(6)(a) ya Katiba ya nchi, inatoa haki ya kukata rufaa. Hivyo Kama ujaridhika na hukumu ya Mahakama ya Wilaya Hai iliyokukuta na hatia , unayo hadi ya kukata rufaa ili Mahakama ione Mahakama Kuu itamke hukumu hiyo iliyokutia hatiani ilikuwa na uhalali wa kisheria au laa.
Mbowe amka usingizini,jitambue wewe ninani?Una madaraka gani?.
Matendo uyatendayo yanayosababisha ufunguliwe Kesi zaidi ya Moja,uitwe Polisi kuhojiwa chini ya Ulinzi Mkali.
Hata kama watu wako wa karibu yako hawakuambii ukweli,minakwambia matendo hayo yanakupunguzia heshima Mbele ya watu wastaarabu Kwani tangu Juzi ulipotiwa hatiani watu wamekuwa wakisema hivi sasa Chadema Inaongozwa na Mwenyekiti Mhalifu na wanahaki ya kukuita wewe ni mhalifu kwasababu Mahakama imekutia na hatia ya Kutenda kosa la kumshambulia mtu.
'Mume wangu wa zamani' ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour(TLP), Augustine Mrema , Mabere Marando, Mwenyekiti wa Chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila, Miaka ya nyuma walifanya sana wazimu huo wa kuvunja Sheria za nchi mwisho wa siku walivyojitambua, na kufahamu madhara ya kukabiliwa na Kesi za jinai mahakamani waliamua kuachana na vitendo vile Vya kiuno Vya kuvunja Sheria za nchi.Jifunze kutoka Kwao maana wamekutangulia kuingia Kwenye ulingoni siasa za vyama Vya upinzani nchini.
Mungu ibariki Tanzania
Chanzo: Blogg: katabazihappy.blogspot.com
Facebook: Happy Katabazi
0716 774494
Juni 19 Mwaka 2015.
Next Post Previous Post
Bukobawadau