MHE. ZITTO KABWE: JANUARY MAKAMBA ASHINDWA KUTAMKA MIIKO YA VIONGOZI
Mheshimiwa
Zitto Kabwe amefunguka katika ukurasa wake wa Facebook na kuweza
kumponda mbunge mwenzake wa Bumbuli, Mheshimiwa January Makamba kutokana
na Hotuba yake aliyoisoma jana katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar
es Salaam wakati akitangaza nia ya Urais wa Jamhuri wa Muungano wa
Tanzania mwaka 2015.
Ujumbe akiyouandika Mheshimiwa Zitto Kabwe...
January
Y. Makamba ndiye mgombea wa CCM aliyejieleza kwa ufasaha zaidi kuliko
wote. 'content' kawazidi wenzake wote. Hata hivyo ameshindwa kabisa
kutamka Miiko ya Viongozi. Bila Miiko yote aliyoyataja hayatafanyika
maana ufisadi utatamalaki. Unaweza kuondoa rushwa kwa sheria. Lakini
huwezi kuondoa ufisadi bila Miiko ya Viongozi. Sijui kwanini Kijana
mwenzangu kaona aibu japo kutaja neno Miiko. Uchaguzi wa mwaka huu
umeegemezwa kwenye kurudi kwenye Misingi iliyoasisi Taifa.
Nimeridhika
sana na content na context. Sikubaliani na mwono. January Makamba
anaiona Tanzania ya kibepari. Nadhani inabidi kufumua uchumi wa kibepari
na kujenga uchumi wa kijamaa. I would love to debate him on the kind of
the nation we shall rebuild. Kila la kheri rafiki yangu.
Maono ya watu waliyoyatoa....
Faraja MG.
Ubepari ndo wenyewe. Ujamaa tulishauzika. Huwezi endelea na Ujamaa.
Jimy Macha
Katumia sana shule kwenye kujieleza kuliko uhalisia.....
Joseph Pjp.
Ingekuwa
tunawapima wagombea kwa kujieleza basi nchi hii #MC wa sherehe
wangefaa kuwa marais wetu! na watunga hotuba kama yeye , hiyo ilikuwa
ajira yake kuandika hotuba.
Kimsingi
January ni uzao wa huo mfumo anaoulalamikia kuwa atauletea Mabadiliko!
#Baba yake amekuwa kwenye same system #iliyofeli anayoilalamikia
kuwa imefeli! for 50 years #genetically he has proved us right kuwa
hana jipya sawa na wazazi wake walivyofeli na yeye amefeli! refer
#simcardTax na tozo ghali za simu , MB 8 , hayo ni mambo madogo tuu
kafeli.
hatujasahau
hiyo sheria ya mitandao aliyekuja nayo ya kuzima moto na sasa haiwezi
kufanya kazi. inshort ni ngumu fisii kuzaa swala!
sio mimi, ni kanuni ya Genetics!
David Mssika.
January
Y. Makamba did well. Maybe hizo kasoro ziwe ni challenge kwake.
Nimependa ufufuaji wa njia za uchumi na mikakati YA kuongeza/kupata
fedha from within! Hii itapunguza dependency syndrome! Kitu nimekosa kwa
wote Usalama wa raia na Mali zao, usalama wa nchi na namna YA kuboresha
demokrasia.
Albert Kamwela.
Nina shaka na utekelezaji. Maneno yanakuwa mengi kuliko utekelezaji.
Goodluck Andrew Msaky.
Hivi
mradi wa MKURABITA ungeenda ipasavyo hawa watia nia wangezungumza kitu
gani? Anatuambia ataunda baraza la mawaziri18 lenye maadili wakati hiyo
sera ilikuwepo kwenye rasimu ya katiba ya Jaji Warioba na ndiyo hiyo CCM
wameipiga vita bungeni akiwemo sasa leo anatuambia kitu gani.. Naona
kama anakosoa yaliyofanywa kipindi cha awamu ya nne na yeye alikua na
uwezo wa kushauri kama naibu waziri mambo yakaenda sawa.
Manywele Omary.
Chui
katika Ngozi ya kondoo.. Nadharia na Vitendo ndo tofauti kubwa kwa
viongozi wa CCM, so far me naona Mwigulu Nchemba ndo yupo na real inner
spirit ya mabadiliko.
Lyaruu Engelbert John.
Ni
mkusanyiko wa yale yale!! Kweli hatujapata jibu la changamoto zetu.
Hawa walikuwa na rais mbona haya wanayoongea hawakufanya katika wizara
zao; au rais hakuwa na utashi! Tujiulize.