Mil. 207 zatumika kupunguza athari za ukame Kishapu
Mratibu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu wa Mradi
wa Kuijengea Jamii Uwezo wa kupunguza Athari za Maafa kwa Mikoa iliyoathirika
zaidi na Ukame, , Harrison Chinyuka
akisisitiza jambo wakati
wa mafunzo ya menejimenti ya maafa kwa Wataalam na waratibu maafa mkoani
Shinyanga tarehe 25, Juni, 2015.
Mratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu maafa, Theodosia Mbunda akifanya majadiliano na washiriki wa mafunzo ya menejimenti ya maafa mkoani Shinyanga wakati wa mafunzo hayo yaliyoratibiwa na Ofisi hiyo kwa waratibu wa Maafa mkoani Shinyanga tarehe 25, Juni, 2015.
Mshiriki wa mafunzo ya Menejimenti ya maafa mkoani Shinyanga, Pastor Mphoy akisisitiza jambo wakati wa mafunzo hayo yaliyoratibiwa na Ofisi hiyo kwa waratibu wa Maafa mkoani humo tarehe 25, Juni, 2015.
Mkuu wa Huduma za Hali ya Hewa kwa Jamii, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, Hellen Msemo, akifanya majadiliano na washiriki wa mafunzo ya menejimenti ya maafa mkoani Shinyanga wakati wa mafunzo hayo yaliyoratibiwa na Ofisi hiyo kwa waratibu wa Maafa mkoani Shinyanga tarehe 25, Juni, 2015.

Na. Mwandishi Maalum.
Serikali kupitia Ofisi ya
Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu maafa imefanikiwa kupunguza athari za maafa
yatokanayo na ukame wilayani Kishapu kwa kutumia jumla ya Shilingi milioni 207 kwa
kutekeleza Mradi wa Kuijengea Jamii Uwezo wa Kupunguza Athari za Maafa yatokanayo
na ukame wilayani humo kwa kuijengea
jamii uwezo wa kupata uhakika wa chakula na kipato.
Mradi huo umetekelezwa kwa mafanikio
katika kata 3 za Mwamalasa, Masanga na Langana, ambapo vikundi vya maendeleo kumi (10) vyenye
jumla ya wanachama 100 vimefanikiwa katika ufugaji wa Mbuzi na kuku, kilimo cha viazi, mtama,
mboga mboga pamoja, upandaji wa miti kwa
uhifadhi wa mazingira na utengenezaji mtandao wa maji safi na salama kwa
matumizi ya binadamu.
Akiongea wakati wa mafunzo ya waratibu maafa na wataalum katika
ngazi za kata, Shinyanga tarehe 25 Juni, 2015, Mratibu maafa
Wilayani Kishapu, Ponsian Kuhabwa amefafanua kuwa fedha hizo zilizotolewa na
Ofisi ya Waziri Mkuu kwa menejimenti ya
maafa ya ukame zimefanikisha kata 3 zinazotekeleza mradi huo kupata uhakika wa
chakula na kipato.
Kuhabwa; “Fedha tulizozipata
katika kipindi cha miezi sita ambacho tumetekeleza mradi huu tumeweza kutoa mafunzo ya menejimenti ya maafa
ya Ukame kwa wataalamu wa ngazi za kata, mafunzo ya Ugani, kununua pembejeo, vifaa na dawa za mifugo, kupitia mradi huu tunao
mbuzi 1050, kuku 1800 ikiwa awali
walipatiwa mbuzi 550 na kuku 550 hali ambayo huzifanya kata hizo kutoathiriwa
na ukame.”
Mkazi wa kijiji cha Masanga,
kata ya Masanga, wilayani Kishapu, Magreth William, amebainisha kuwa ukame
uliokuwa ukiikumba kata hiyo mara kwa mara, walikuwa wanapata athari za
upungufu wa chakula pamoja na kutokuwa na kipato kutokana na mazao yao ya
biashara kuharibikia mashambani.
William; “Tumeweza kupunguza
athari za maafa ya ukame kupitia mradi huu kwa kuwa tunao uhakika wa chakula
kwa kuwa tunalima mazao yanayo himili ukame kama mtama na viazi lishe lakini
pia tunao uhakika wa kipato kwa kuwa tunafuga mbuzi na kuku hivyo pamoja na
ukame unaendelea kujitokeza lakini kwa sasa hatuathiriki kama awali”.
Mradi wa Kuijengea
Jamii Uwezo wa Kupunguza Athari za Maafa kwa Mikoa iliyoathirika zaidi na ukame
unafadhiliwa na Benki ya Dunia na kusimamiwa na UNICEF chini ya uratibu wa
Ofisi ya Waziri Mkuu na Halmashauri husika wakiwa Watendaji wakuu wa mradi huo.
Mradi huo unatekelezwa kwa kipindi cha miezi 18, ulizinduliwa wilayani Same, mkoani Kilimanjaro tarehe 11 Desemba,
2013.