PAPA MSOFFEPAPA MSOFFE AFUTIWA KESI YA MAUJI LEO
Na Happiness Katabazi
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imemfutia kesi ya Mauji iliyokuwa ikimkabili mfanyabishara maarufu
Marijani Abdubakari Msoffe baada ya kupokea taarifa toka kwa
MKurugenzi wa Mashitaka (DPP) , Biswalo Mganga Leo Kuwa Hana nia ya kuendelea kumshitaki tena.
Kwa mujibu wa Kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002 ,inampa mamlaka DPP kuifuata kesi ya jinai bila kuhoji wa na mtu yoyote wala mamlaka yoyote ile.
Hata hivyo dakika Chache baada ya Kufutiwa Kesi hiyo ya mauji kinyume na Kifungu cha 196 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya Mwaka 2002 ambapo kisheria Mahakama ya Kisutu ilikuwa haina mamlaka ya kuisikiliza na haina dhamana na hivyo kwa Kipindi chote hicho tangu Agosti 10 Mwaka 2012 hadi Leo alikuwa akiishi Gereza la Keko Kisha aamishiwa gereza la Ukonga .
Leo pia upande wa Jamhuri umemfungulia Kesi mmoja ya kughushi Nyaraka za Viwanja ambayonendapo akitiiza Masharti ya dhamana anapata dhamana na hivyo kurudi nyumbani kwake kuungana na familia yake.
Hata hivyo hadi sasa bado hajatekeleza Masharti ya dhamana bado yupo chini ya Ulinzi Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Pole Msoffe na hongera kwakufutiwa Kesi hiyo Ndio Sheria lazima ifutwe na wale waliopewa jukumu la kusimamia na kutekeleza Sheria.Na Imani kwa kupata tuhuma zile za Kesi za Mauji na kukasababisha ukaishi gerezani ni wazi utakuwa umejifunza sasa Kuwa Sheria zipo ,hazibagui masikini wa Tajiri wala Mtu maarufu,na dola linanguvu sana kuliko mwananchi wa aina yoyote yule na linamkono mrefu .
Ushauri wangu jiepushe kukaribia au Kutenda mambo yanavunja Sheria.
Msoffe ambaye wewe ni shabiki mwenzangu wa Bendi ya FM academia nakushauri kaa mbali na tuhuma mbaya ambazo umekuwa ukisifika nazo sina haja ya kuzitaja hapa.
Nakumbuka Uliwahi kushitakiwa kwa Kesi Moja katika Mahakama ya Kisutu ukaenda Jela kwa kukosa dhamana na Kesi ile ikaisha ila Kesi hii ya Mauji ilisababisha licha na Umaarufu wako wote Ukaa Jela kwa Kipindi chote hicho.
Nimelazimika kuandika story hii ya Msoffe Kufutiwa Kesi hii Kwani Mimi nilikuwa ni miongoni mwa waandishi wa Habari tuliokuwa siku ya kwanza anafikishwa mahakamani hapo kuandika Habari yake mfululizo hadi baadhi ya ndugu zake wakawa wanatuzuia tusimpige picha na kututolea maneno machafu bila kujua tulikuwa tukitimiza wajibu wetu hadi nilipoachakazi ya uandishi wa habari katika gazeti la Tanzania Daima Agosti mwaka 2014 ndipo nilipoacha kuandika kesi hii.Tulishawasamehe.
Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
24/6/2015