SERIKALI ZA VIJIJI ZATAKIWA KUHUSISHA MAAFA YA MABADILIKO YA TABIANCHI NA MIPANGO YA MAENDELEO
Mshiriki
wa Mafunzo ya utekelezaji mradi wa Kuimarisha mfumo wa
habari za hali ya hewa na mifumo ya tahadhari ya mapema nchini akichangia
wakati wa mafunzo hayo kwa wajumbe wa kamati za maafa za kata ya Makiba,
wilayani Arumeru mkoani Arusha, mafunzo hayo yameratibiwa na Ofisi ya Waziri
Mkuu kupitia mradi huo , Tarehe 13 Juni, 2015.
Mratibu mradi kitaifa wa Kuimarisha mfumo wa habari za hali ya hewa na mifumo ya tahadhari ya mapema nchini, Alfei Daniel akifafanua jambo wakati wa mafunzo ya utekelezaji wa mradi huo kwa wajumbe wa kamati za maafa za kata ya Makiba, Wilayani Arumeru mkoani Arusha, tarehe 13 Juni, 2015, wengine ni wawezeshaji wa mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo ya utekelezaji mradi wa Kuimarisha mfumo wa habari za hali ya hewa na mifumo ya tahadhari ya mapema nchini, kutoka kamati za maafa za kata ya Makiba, wilayani Arumeru mkoani Arusha, wakiandika maudhui ya mafunzo hayo yaliyoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Tarehe 13 Juni, 2015.
Washiriki kutoka kamati za maafa za kata ya Makiba, Wilayani Arumeru mkoani Arusha, wakiwa katika picha ya pamoja na Mratibu mradi kitaifa wa Kuimarisha mfumo wa habari za hali ya hewa na mifumo ya tahadhari ya mapema nchini, Alfei Daniel (wa kwanza kushoto) mara baada ya kufunga mafunzo ya utekelezaji wa mradi huo, tarehe 13 Juni, 2015.

Serikali
za vijiji zatakiwa kuhusisha Maafa ya mabadiliko ya tabianchi na mipango ya
maendeleo.
Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara
ya Uratibu Maafa kupitia
mradi wa kuimarisha mifumo ya
habari za hali ya hewa na mifumo ya tahadhari nchini imezitaka serikali
za mitaa
na vijiji nchini kuhusisha maafa yatokanayo na mabadiliko ya tabianchi
na mipango yao ya maendeleo, ili kuhakikisha jamii inakuwa na uchumi bora na
uwezo wa kupunguza athari za maafa hayo.
Akiongea wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wajumbe
wa Kamati ya Maafa wa kata ya Makiba Wilayani Arumeru, mkoani Arusha, Mratibu
Mradi huo Kitaifa, Alfei Daniel tarehe 13 Juni, 2015, alisema serikali za vijiji zitumie
taarifa za athari za mabadiliko ya tabianchi za vijiji vyao ambazo zitakuwa
zinaainishwa kupitia mradi huo kama
sehemu ya kuandaa mipango mikakati ya maendeleo vijijini.
“Kupitia mradi huu tutakuwa
tunatoa taarifa za hali ya hewa kwa eneo husika na kwa wakati, Ufahamu juu ya Hali ya hewa, mabadiliko ya tabianchi, maji
na mazingira ni muhimu sana na ni kiungo
kikubwa katika kuandaa mikakati na mipango ya maendeleo vijijini, hii itasaidia
kuimarisha uwezo wa serikali za vijiji kuwalinda wananchi kwa athari
zinazoweza kusababishwa na mabadiliko ya tabianchi” alisisitiza Daniel
Aliongeza kuwa uwepo wa miundombinu
hafifu vijijini, upungufu wa wataalamu wa masuala ya hali ya hewa pamoja na taarifa
za hali ya hewa kutowafikia wanavijiji kwa wakati, kumekuwepo na matumizi
madogo ya taarifa za hali ya hewa kitendo ambacho huziweka jamii za vijijini
katika mazingira magumu hasa kwenye shughuli za kiuchumi pindi yanapotokea
maafa ya mabadiliko ya tabianchi kama ukame na mafuriko.
Akiogea wakati wa mafunzo
hayo Diwani wa Kata ya Makiba, Wilayani Arumeru Mkoani Arusha, Mwanaidi Kim
alifafanua kuwa ni muhimu vijiji kuhusisha maafa yatokanayo na maafa ya
mabadiliko ya tabianchi katika mipango ya maendeleo kwani athari zake
zinapotokea shughuli za maendeleo hukwama.
“Katika kata yangu kuna
vijiji sita ambavyo ni; Makiba, Patanumbe, Valesika, Engatani na Kaloleni,
lakini katika vijiji hivi vyote kuna ishara ya upungufu wa chakula, Hivyo kama
mtu hana chakula ni vigumu kufanya shughuli za maendeleo lakini kupitia mradi huu athari hizi hazitatupata tena
kwani tutakuwa tunapata taarifa za hali ya hewa kwa wakati na sisi
tunapanga vizuri mipango yetu ya kimaendeleo” alisema
Mradi huo ambao
utatekelezwa nchi nzima, kwa sasa unatekelezwa kwa majaribio tangu mwaka 2014 hadi
2018 katika Halmashauri ya wilaya ya Meru, Mkoani Arusha na Halmashauri ya wilaya ya Liwale, mkoani
Lindi.