WASANII KUTUMIKA KUELIMISHA UMMA MENEJIMENTI YA MAAFA
Askari wa Jeshi la Zima moto
nchini, Josephat John akieleleza matumizi ya Kizimamoto wakati wa mafunzo ya
menejimenti ya maafa kwa watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, mjini Dodoma
tarehe, 21 Juni, 2015.
Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia mafunzo ya majanga ya moto wakati wa mafunzo ya menejimenti ya maafa mjini Dodoma tarehe, 21 Juni, 2015.
Afisa Tawala, Ofisi ya
Waziri Mkuu, Leah Kibassa, akifanya mazoezi ya kutumia kizima moto wakati wa
mafunzo ya menejimenti ya maafa kwa watumishi wa Ofisi hiyo, mjini Dodoma
tarehe, 21 Juni, 2015.
Mkurugenzi wa Idara ya
Uratibu Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu,
Brig. Jen. Mbazi Msuya (mwenye tai) akishuhudia, Salma Juma akikabidhiwa Kizima
moto kilichonunuliwa na washiriki wa mafunzo ya menejimenti ya maafa wa Ofisi
hiyo mjini Dodoma tarehe, 21 Juni, 2015,
Kwa lengo la kuhamasisha watumishi wa Ofisi hiyo kukabili majanga ya
moto,Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia mafunzo ya majanga ya moto wakati wa mafunzo ya menejimenti ya maafa mjini Dodoma tarehe, 21 Juni, 2015.
Wasanii
kutumika kuelimisha umma menejimenti ya maafa
Na.
Mwandishi Maalum
Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara
ya Uratibu maafa inaandaa mkakati wa elimu kwa umma wa menejimenti ya maafa ambao
utawatumia watu maarufu nchini wakiwemo wasanii wa sanaa mbali mbali kwa lengo la kufikisha elimu kwa umma ya
menejimenti ya maafa.
Akiongea wakati wa mafunzo
ya menejimenti ya maafa kwa watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mjini Dodoma
mwishoni mwa wiki hii, Brig.Jen, Mbazi Msuya alibainisha kuwa jamii
ikielimishwa kikamilifu juu ya menejimenti ya maafa athari za maafa zinapunguzika.
“Tunaposema menejimenti ya
maafa tunazingatia, kuzuia, kukabili
maafa na kurejesha hali ya awali baada ya maafa kutokea. Kwa mantiki hii
kama tunavyo elewa Wasanii wanao uwezo
wa kufikisha ujumbe kwa haraka, lugha nyepesi, kwa watu wengi na kwa ujumbe mmoja, hili ndo linalotusukuma
kufikiria kutumia hawa watu katika kutoa elimu ya menejimenti ya maafa kwa
jamii yetu” alisema Msuya.
Msuya aliongeza kuwa nchi
yetu imekuwa ikikumbwa na majanga ya asili
na yale yanayosababishwa na binadamu, ambapo majanga yanayosababishwa na
binadamu kwa kiwango kikubwa jamii inaweza
kuyakabili tu ikiwa elimu ya
menejimenti ya maafa hayo imemfikia kila
mwanachi. Hivyo kwa kuwa wasanii wengi msingi wa kazi zao za sanaa huaksi
yanayojiri katika jamii yao hivyo hii itakuwa ni fursa kwao kuijengea jamii
uwezo wa kuyakabili maafa.
“Athari za Majanga yanayosababishwa
na binadamu kama moto yanaweza kuzuilika ikiwa menejimenti ya majanga hayo
itatolewa kwa umma. Wananchi wakielimishwa umuhimu wa kuwa na vizima moto
majumbani mwao na katika vyombo vya moto wanaweza kukabili majanga ya moto na
hili litawezekana kwani tayari tunayo mikakati ya mawasiliano ya kukabiliana na
maafa ” alisisitiza Msuya.
Ofisi ya waziri Mkuu kupitia
Idara ya Uratibu maafa tayari imeshaandaa Mkakati wa Mawasiliano wa kukabiliana na maafa
kwa mkoa wa Mtwara, Shinyanga na Dodoma
lengo ikiwa ni kila mkoa nchini kuwa na mkakati huo utakowezesha menejimenti ya
maafa kwa jamii ya watanzania. Aidha mkakati huo unabainisha kila mdau wa maafa
wajibu wake katika menejimenti ya maafa wakiwemo wasanii.