YANINI KUWATAJATAJA MBELE ZAKE??
Inasumbua sana moyo pale ambapo mpenzi wako kila mkiongea au kila
akikukosoa anakulinganisha na mpenzi au wapenzi wake wa zamani, utaskia
anasema "hata nanihii niliachana naye kwa tabia hiyohiyo" hivi kama
unataka kumrekebisha mwenzako lazima umtajie hao wapenzi wako wa
zamani??? Kama hawajakutoka moyoni mbona umeanza mapenzi mengine? We
fahamu kwamba mwenzako anaumia - Chris Mauki.