BREAKING NEWS:MAJINA NI BERNARD MEMBE, MAGUFULI,MIGIRO,MAKAMBA NA AMINA S.ALI
Kikao cha KAMATI KUU (CC) kimekamilika na kufanikiwa kuwateua wagombea wake 5 ambao ni…Bernard Membe , John Magufuli , Asha Rose Migiro, January Makamba na Amina S. Ali
DODOMA: Tovuti ya CCM imeyatangaza majina matano yaliyopitishwa na Kamati ya CCM (CC) kuwa ni Bernard Membe, John Magufuli, Asha-Rose Migiro, January Makamba na Amina S Ali
7:00 Kamati Kuu ya CCM imeeenda mapumziko mafupi kwa ajili ya Kufuturu na watarejea tena majira ya saa mbili usiku.
DODOMA: Tovuti ya CCM imeyatangaza majina matano yaliyopitishwa na Kamati ya CCM (CC) kuwa ni Bernard Membe, John Magufuli, Asha-Rose Migiro, January Makamba na Amina S Ali
12:55 Kikao cha Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi
(CC) kimemalizika hivi punde mjini Dodoma na Katibu wa Itikadi na Ueneze
Nape Nnauye ameshindwa kutaja majina matano ambayo yatapelekwa kwenye
Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho (NEC)
Badala yake amewaambia waandishi wa habari kuwa majina hayo yatatangazwa saa nne asubuhi.
Aidha kwa mujibu wa Matangazo yaliyorushwa moja
kwa moja na kituo cha redio Uhuru, Sophia Simba alisikika akisema kuwa
mvutano mkali ulikuwemo ndani kikao hicho na wajumbe, Adam Kimbisa, Dk
Emmanuel Nchimbi na yeye mwenyewe hawakukubaliana na maamuzi ya kikao
yaliyofikiwa.
10:10 Bado kikao cha Kamati Kuu (CC) kinaendelea
taarifa zilizopo ni kwamba kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC)
kimeahirishwa hadi kesho saa nne asubuhi
8:12 Kikao cha Kamati Kuu kinarudi kuendelea na
kitatoa taarifa ya majina matano ambayo kwa sababu ya muda yatajadiliwa
kesho na Kikao cha Halmashauri na Mkutano Mkuu utafanyika kesho mchana,
Kwa mujibu wa Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
7:00 Kamati Kuu ya CCM imeeenda mapumziko mafupi kwa ajili ya Kufuturu na watarejea tena majira ya saa mbili usiku.
4:30 KUMEKUCHA Dodoma, Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeanza mkutano wake wa Kamati Kuu saa chache zilizopita.
Taarifa kutoka Dodoma zinasema watu wote
wameondolewa ndani ukumbi mpya wa CCM ikiwa ni pamoja na waandishi wa
habari ambapo hivi sasa wanasubiri taarifa hizo nje ya ukumbi huo.
Endelea kuwa nasi kwa habari zaidi kutoka Dodoma ......
Breaking News: Dr.Nchimbi,Sophia Simba na Adam Kimbisa: "Katiba ya chama imekiukwa.Hawaungi mkono maamuzi ya Kamati Kuu" #Dodoma