GLOBAL EDUCATION LINK YAVIALIKA CHUO KIKUU CHA SHARDA NA LOVELY PROFESSIONAL VYA INDIA KUSHIRIKI MAONYESHO YA SABASABA JIJINI DAR
Mkurugenzi wa Global Education Link ambao ni Mawakala wa Vyuo Vya Nje
ya nchi, Bw. Abdulmalik Mollel (wa pili toka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa vyuo vya nje ya nchi kutoka kushoto ni Meneja Miradi wa Chuo Kikuu cha Lovely Professional cha Nchini India, Bw. Gulshan Sandh na Bw. Sourabh Chaudhary pamoja na Meneja wa Kanda wa Chuo Kikuu cha Sharda cha nchini India, Bw. Deepak Kaushik mara baada ya kuwakaribisha katika ofisi yao iliyopo ndani ya maonyesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba yanayofanyika viwanja
vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Global Education Link ambao ni Mawakala wa Vyuo Vya Nje ya nchi, Bw. Abdulmalik Mollel (wa pili toka kulia) akiongea na wageni wake ambao ni viongozi wa vyuo vya nje mara baada ya kuwaalika kushiriki katika maonyesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Principal Academic Officer wa Chuo cha IFM cha jijini Dar es Salaam akisisitiza jambo la kielimu wakati alipokutana na viongozi wa vyuo vya nje ya nchi ndani ya ndani ya ofisi za GEL zilizopo ndani ya maonyesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG.